Na Dotto Mwaibale
BODI ya
Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi kesho kutwa inatarajia
kuendesha semina ya siku moja kwa ajili ya kuwanoa wadau wa sekta ya ujenzi
nchini.
Hayo
yamebainishwa na Msajili wa Bodi hiyo, Jehad Jehad wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu semina hiyo muhimu itakayofanyika kesho kutwa ukumbi
wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
"Semina
hii ambayo ni ya 26 ni muhimu sana kwetu sisi watu wa sekta ya ujenzi
hasa katika kipindi hiki ambacho taifa linatutegema" alisema Jehad.
Alisema
semina ya namna hiyo zilianzishwa tangu mwaka 2003 na hufanyika mara mbili kwa
mwaka ambapo jumla ya wabunifu majengo, wakadariaji majenzi na wadau
wengine wa sekta ya ujenzi wapatao 5,328 wamekuwa wakinufaika na semina hizo.
Alisema
malengo ya semina hiyo ni kuwanoa wabunifu majengo na wakadariaji majenzi na
wadau wengine katika sekta ya ujenzi kutambua fursa ambazo ziko katika soko la
Afrika Mashariki (EAC) na lile la Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa
Afrika (SADC)
Alitaja lengo jingine kuwa ni
kuwafahanisha wadau faida na umuhimu wa sheria ya mtandao katika kuboresha
huduma zao kwa wananchi na kubadilishana uzoefu wa kazi zao za kitaaluma kwa
lengo la kuongeza weredi pamoja na kuwapa fursa waataamu katika sekta ya ujenzi
kupata nasaha kutoka kwa viongozi wa Serikali.
Jihad aliswema katika semina hiyo mada
mbalimbali zitatolewa na kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi, Jehad A. Jehad (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu semina ya 26 siku moja itakayo washirikisha wadau wa Sekta ya ujenzi itakayofanyika kesho kutwa Septemba 22, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Ambwene Mwakyusa.
Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadriaji Majenzi wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Utawala, Angelo Ngalla, Mwanasheria, Ibrahim Mohamed na Ofisa Uhusiano, Hamisi Sungura.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...