THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAKALA ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuendesha kampeni maalum ya kupima matumizi ya vilevi

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam

WAKALA ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekusudia kuendesha kampeni maalum ya kupima matumizi ya vilevi kwa madereva wanaosafirisha abiria na mizigo ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wadau wa kemikali juu ya matumizi salama ya kemikali nchini.

Prof. Manyele alisema utaratibu wa kuwapima madereva hao utaanza hivi karibuni na utawezesha kupunguza tatizo la ajali barabarani na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushirikiano katika zoezi hilo.

“Madereva wote wanaosafirisha mizigo na abiria  watatakiwa kupita kwenye kipimo ambacho kitaonyesha kama madereva hao wanatumia vilevi, hali hiyo itasaidia kutatua tatizo la ajali za barabarani nchini”, amesema Prof. Manyele.

Aidha, Prof Manyele alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kutoa uwezo na uelewa kwa wahusika  hasa wasimamizi wa shughuli za kemikali na matumizi salama juu ya kukabiliana na matukio au ajali za kemikali pale yanapotokea.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yamekuja kufuatia uelewa mdogo wa elimu kwa baadhi ya wadau wanaojishughulisha na masuala ya kemikali kuhusu uzalishaji, uhifadhi, usimamizi na usafirishaji wa matumizi ya kemikali nchini.

Mbali na hayo, Prof Manyele alisema kumekuwa na ajali na matukio yanayotokana na kemikali ikiwemo ya ajali halisi na mengine kutokana na kukosa uelewa wa matumizi sahihi na salama ya kemikali.


Akifafanua zaidi Prof. Manyele alisema katika kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi yasiyo salama ya kemikali, Serikali ilitunga sheria ya Kemikali za Viwandani na majumbani mwaka 2003 kwa lengo la kuhakikisha kemikali hizo zinatumika katika hali iliyo salama.