THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WAKURUGENZI WATEULE KUWASILI DODOMA,KULA KIAPO CHA UADILIFU WA UONGOZI WA UMMA SEPTEMBA 13


Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma.

Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Manispaa na Wilaya, walioteuliwa siku ya Jumamosi Septemba 10, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wametakiwa kuwasilisha nakala halisi za vyeti vyao vya taaluma, kabla ya kuapa.

Zoezi la uhakiki wa vyeti hivyo litakalofanyika Ofis ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika jengo la Mkapa mjini Dodoma siku ya Jumanne Septemba 13, 2016 kabla ya kuanza kwa zoezi la kuapa.

Wakurugenzi hao 13 ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa mmoja, Mkurugenzi wa Mji mmoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, wanatakiwa kuwasili Ofisi ya Rais TAMISEMI mjini Dodoma saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya uhakiki wa vyeti vyao vya taaluma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe na kusainiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Rebecca Kwandu, Septemba 11, 2016 inawataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanawasilisha nakala halisi ya vyeti vyao vya taaluma kwa ajili ya kiapo cha uadilifu wa uongozi wa umma.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa uhakiki wa vyeti halisi vya kitaaluma, unafanywa kwa lengo la kujiridhisha baada ya mchakato wa kawaida wa uhakiki kufanywa kwa kutumia vyeti visivyokuwa halisi yaani vivuli.

Wakurugenzi hao ni Godwin Emmanuel Kunambi Manispaa ya Dodoma, Elias R. Ntiruhungwa Mji waTarime, Mwantumu Dau Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Frank Bahatui Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Hudson Stanley Kamoga Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mwailwa Smith Pangani, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Godfrey Sanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na Yusuf Daudi Semuguruka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.

Wakurugenzi wengine ni Bakari Kasinyo Mohamed Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Juma Ally Mnweke Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Butamo Nuru Ndalahwa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Waziri Mourice Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Fatma Omar Latu Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.