THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi aongoza matembezi ya hisani kuchangia waathirika wa tetemeko Kagera, yachangisha shilingi bilioni 1.5

Na: Frank Shija, MAELEZO
TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu mjini Bukoba Mkoani Kagera.
Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.
“Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.
Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.
“Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.

Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.
Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.
Baadhi ya washiriki wa  hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= zilipatikana. 
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Katika matembezi hayo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kimepatikana. 
 Wawakilishi wa Jumuiya ya Wabohora nchini  wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera kwa Rasi wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Bw. William Erio na Afisa Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Waziri wa Mmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashari katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya “ Walk for Kagera” Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Busemaker akipokea cheti kwa ajili ya kutambua udhamini wa Benki hiyo katika kufanyikisha matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Kagera leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA