Mwenyekiti wa Dr. Amon Foundation Bw. Amon Mkoga  ametoa mchango wa madawati  katika kampeni ya uchangiaji madawati  kwa udhamini wa mtandao wa simu za mkononi wa Halotel hii leo katika ukumbi wa Idara ya Habari  Maelezo jijini Dar-es-Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Amon Mkoga amesema kuwa ili kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ,wameandaa kampeni ya “Simama Kaa Desk” Kampeni.,  itakayosaidia kupunguza uhaba wa madawati mashuleni.

“Lengo kubwa la kampeni hii ya “Simama Kaa Desk”   ni kuchangia na kupunguza upungufu  wa madawati katika shule za msingi na sekondari  ili kumuunga mkono rais wa  Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, Kampeni hiyo  itaanzia katika mkoa wa Tabora na Pwani.”

Aidha afisa mawasiliano wa Halotel Stella Pius amesema kuwa Halotel itakuwa pamoja na Dr Mkoga Foundation kuhakikisha kwamba watakuwa bega kwa bega ili kuwasilisha mchango wa madawati katika elimu.

Licha ya hayo pia kutakuwa na burudani ya muziki wakati wa kukabidhi madawati hayo ambayo italetwa na  kundi la muziki wa kizazi kipya la Mabaga Fresh la jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Dr. Amon, Amon Mkoga (katikati) , Ngo Duy Truong Meneja Masoko Halotel, Kushoto na Stella Pius Meneja Mawasiliano wa Halotel wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa idara ya habari Maelezo, jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...