THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

WASHIRIKI 10 WAINGIA FAINALI KATIKA SHINDANO LA GOSPEL STAR SEARCH 2016 JIJINI DAR

Kikundi cha Makerubi kutoka Manyara ambao walijiandikisha wakitokea Temeke waliweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika shindano la Gospel Star Search 2016 kwa kuweza kuimba kwa ustadi mkubwa. Shindano la Nusu fainali lilifanyika katika viwanja vya Biafra - Kindononi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
 PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano mkali.
Kiongozi wa Majaji, Mchungaji Sam Mwangati akisoma majina ya vijana walifanikiwa kuingia hatua ya fainali ya shindano la Gospel Star Search 2016 lililofanyika katika uwanja wa Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Fainali za shindano hili zinatarajiwa kufanyika jumapili ya Septemba 18, 2016 katika ukumbu wa Milado, Sinza jijini Dar es Salam. 

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason blog. 
 Vijana 10 wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali katika shindano la kumtafuta mkali wa kuimba nyimbo za injili 'Gospel Star Search 2016' lililofanyika katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Akizungumza Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali alisema kuwa ni vyema vijana wakazingatia mafundisho yote waliyopatiwa na walimu wao ili waweze kushindana kwa uweledi na ustadi wa hali ya juu.

 Alisema wakati umefika wa vijana kutambua talanta au vipaji walivyopewa na mwenyezi Mungu ili viwaletee manufaa katika kumtangaza Bwana Yesu Kristo. "Tokea tumeanza kuzunguka kukusanya vijana hakika tumeweza kupata vijana wengi wenye vipaji na kuonyesha kuwa mwamko wa vijana katika kutambua vipaji vyao umekuwa mkubwa, hakikuwa jambo jepesi sana ila yote kwa yote tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyeweza kufanikisha yote",  alisema Sasali.

 Aliongeza kuwa shindano la Gospel Star Search 2016 liliweza kupata washiriki wengi ila wakafanyiwa mchujo na kupatikana wapatao 15 ambao waliweza kuingia hatua ya nusu fainali na wakafanya mchuzo katika viwanja vya Biafra wakapatikana 10 ambao wameingia katika kikaango na ipatapo Septemba 18, 2016 Jumapili katika ukumbi wa Milado, Sinza ndipo fainali zitakapofanyika. Vijana 15 waliokuwa wameingia nusu fainali ni 1. Makerubi,  2. Enighenja Mmbaga, 3. Upendo John, 4. Grace Madole,   5. Winnypraise William, 6. Willansia Lema, 7. Rogate Kalengo, 8. Suleiman Wilson, 9. Innocent Eliya. Wengine ni 10. Flora Kachema, 11. Steve Njama, 12. Winnifrida Dudu, 13. Calvin John, 14. Sunday Lunkombe na 15. Beda Andrew. Waliofanikiwa kuingia Fainali ni vijana 10 ambao ni 1. Makerubi, 2. Beda Andrew, 3. Winnypraise William, 4. Rogate Kalengo, 5. Suleiman Wilson, 6. Flora Kachema. Wengine ni 7. Steve Njama, 8. Winnifrida Dudu, 9. Calvin John na 10. Sunday Lunkombe. Shindano la GSS limedhaminiwa na Maendeleo Bank,  Grace Product, Brand exponetial, Kiango media, Clouds Media Group, Fm studios (Faith music lab) na 3D.