Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi, lililoukumba Mkoa wa Kagera hivi karibuni. Mchezo huo utafanyika kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Kabla ya Mchezo huo, kutakuwa na michezo ya Utangulizi ambapo Timu ya Bunge ya Mchezo wa Pete (Netball) inakutana na Timu ya TBC huku Mchezo mwingine ukiwa ni ni kati ya Wasanii wa Bongo Movie na Bongo Fleva. 
Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkeyenge akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi, lililoukumba Mkoa wa Kagera hivi karibuni. Nkeyenge amewataka wale wote watakaojitokeza kwenda kuangalia mchezo huo, wanatakiwa kuwa na tiketi za Kielekroniki ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia hiyo kesho, Pia amezungumzia hali ya usalama katika Uwanja huo kuwa itaimarishwa vizuri kwani Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha hatuna tukio lolote la uvunjifu wa amani litakalojitokeza uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akionyesha moja ya vikombe vitakavyokabidhiwa kwa timu zitakazoshinda katika michezo hiyo ya kesho.
Mwenyekiti wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10, kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication LTD, Francis Nanai ikiwa ni sehemu ya Mchango wao katika kufanikisha zoezi hilo.

WAKATI tiketi za elekroniki zitaanza kujaribio welo, Makampuni mbali mbali wamechangia jumla ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kudhamini mchezo wa wabunge mashabiki wa Yanga na wale wa Simba utakaofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.

Makampuni hayo ni Mwananchi Communication iliyotoa Sh milioni 20, mfuko wa bima ya afya NHIF na Jubilee Insurance ambazo zote zimetoa Sh milioni 5 kila mmoja.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge William Ngeleja ambaye pia ni mnazi wa Simba alisema matokeo ya mchezo wa kesho ni hishara ya matokeo ya mchezo wa Oktoba Mosi.

Nae Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la kusimamia mfumo huo, Gallus Runyeta amesema kadi  hizo zitatolewa bure katika mchezo wa leo ikiwa ni  majaribio na kuangalia dosari ambazo zitajitokeza kabla ya kuanza kuzitumia rasmi. 

Akizungumzia jinsi ya kuitumia kadi hiyo, Runyeta alisema “Utajisajili kwa kupiga *150*50# halafu ni lazima uiwekee pesa kwa Airtel au M-Pesa. Kiwango cha chini cha kuongeza salio ni Sh 1,000….: “ “Unaweza ukanunua mechi moja kwa kuandika tarehe na mchezo husika au ukachagua baadhi ya mechi au ukanunua mechi zote za msimu za timu unayoipenda.

“Unapokwenda kuingia uwanjani, utaweka kadi yako kwenye alama husika na mlango utafunguka wenyewe. Ukishaangalia mechi uliyoinunua, hauwezi kesho yake ukaenda kutazama mechi nyingine ambayo hujailipia. Kadi itasoma kwenye mechi zilizolipiwa tu. Ukiingia uwanjani hauwezi ukatoka halafu ukarudi kwa tiketi ileile. 

Viingilio vya mchezo huo utakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko kijani na bluu, 10000 na 15000  kwa  viti vya machungwa, VIP A 200,000, VIP B 100,000 na VIP C ni 50,000 huku kutakuwa na viti 50 vilivyotengwa ambapo kwa yoyote atakayekaa hapo atalipia 1,000,000.

Katika mchezo huo mbali na wabunge pia kutakuwa na mechi ya bongo movie na bongo fleva ambapo kikosi cha bongo movie kitaongozwa na King Majuto, Dr Cheni, Check Budi, Muhogo Mchungu na Ray Kigosi wakati kwa upande wa Bongo Fleva kitaongozwa na Rich One, Kalla Pina, Ally Kiba, Stamina, KR Muller na H baba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...