THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Wateja wa Vodacom wachangia wahanga zaidi ya laki 4 kupitia M-PESA

Watanzania wawachangia wahanga wa tetemeko Kagera,zaidi ya laki 4 kupitia huduma ya M-Pesa mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya uchangiaji ya”Red Alert”inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Kampuni hiyo ilikabidhi  jumla ya sh.milioni 100/- kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea kanda ya ziwa septemba 10 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es salaam jana  Mkuu wa   kitengo cha Vodacom Tanzania Foundation, Renatus Rwehikiza alisema kati ya fedha hizo zilizochangwa mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni ya uchangiaji wa waathirika wa tetemeko hilo  sh. Mil 99.51 zilitolewa na kampuni yake na sh. 490,000 zilichangwa na watanzania  kupitia M-Pesa.

“Kiasi kilichochangwa na wasamaria wema ni sh 490,000 na sisi  Vodacom tukatoa sh,mil 99.51  ambazo zilijumlimshwa na kupatikana sh mil 100/-ambazo hundi yake ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu  Septemba 24 mwaka huu na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao mara baada ya kampeni ya uchangiaji  kuhitimishwa”alifafanua Rwehikiza.

Aidha Rwehikiza alibainisha kuwa  awali Taasisi yake ilipanga kununua vifaa mbalimbali kwaajili ya kuwasaidia waathirika hao lakini kwa kuwa  Kamati ya Maafa Bukoba ambayo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa  ilikuwa na uhitaji wa fedha zaidi tuliona ni bora tukabidhi fedha.

Katika hatua nyingine Rwehikiza alitoa wito kwa watanzania ,mashirika na Taasisi mbalimbali nchini kuendelea kujitoa katika kuchangia waathirika wa tukio hilo badala ya kuiachia serikali pekee kwani bado uhitaji ni mkubwa.