Kaimu Mkurugenzi wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dkt. Othman  Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya  ya Arusha
Mhe. Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto amefanyiwa upasuaji wa kichwa


 kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman  Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji
 mkuu wa wilaya ya Arusha mjini akimkabidhi pampas moja ya mama mzazi wa mtoto ambaye amefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa ikiwa ni moja ya zawadi walizopatiwa na GSM Foundation

 mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa kikubwa


Na Woinde Shizza, Arusha

Jumla ya watoto 4,000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji huku wengine 3500 haijulikani wanapopelekwa.


Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu  Muhimbili (MOI) Dkt. Othman  Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari Mkoani hapa.

Alisema kuwa  wao kama taasisi ya MOI  walikaa chini na kuona kuna watoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho amesema si kweli.

Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.

"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma

Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Wa kichwa Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada .

"Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa mud a mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto ,tusisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua ,tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.

Naye Mkuu wa wilaya ya Arusha  Mhe. Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususan  wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa .

Aliwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna gani wanaweza kusaidia watoto  hawa pamoja na shirika la GSM foundation ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure  ambapo alisema kwa upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa fanyiwa upasuaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...