Mabaki wa Gari ndogo aina ya Toyota Hiace iliyogongana na Basi la Super Shem jijini Mwanza mapema leo asubuhi, watu 11 wanadhaniwa kupoteza maisha kwenye ajali hilo. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wanaeleza kuwa Basi hilo liliigonga gari hiyo ndogo ambayo iliingia kwenye barabara kubwa bila ya kuwa na tahadhali, hivyo basi hili ambalo lilikuwa kwenye mwendo wa kasi likaigonga. Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza zinaendelea kufanyika ili kuthibitisha tukio hilo.
Muonekano wa Gari hiyo ndogo aina ya Toyota Hiace baada ya kupata ajali hiyo.
Basi la Super Shem linavyoonekana kwa mbele baada ya kugongana na Gari hiyo ndogo aina ya Toyota Hiace.
Wasamalia wakifanya juhudi za kumuokoa Dereva wa Basi hilo aliyekuwa amenasia kwenye usukani baada ya Ajali hiyo.
Sehemu ya Mabaki ya Gari ndogo iliyogongana na Basi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...