THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Waziri Nape aipongeza Kilimanjaro Queens mabingwa kombe la CECAFA


Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewapongeza Wachezaji wa Kilimanjaro Queens kwa niaba ya serikali na kwa niaba ya watanzania kwa kazi nzuri waliyoifanya mpaka kuwa mabingwa wa kwanza wa Kombe la CECAFA kwa mpira wa miguu kwa wanawake Afrika Mashariki na Kati.Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Nnauye alipokua akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

“Kama serikali ni vyema kuipongeza timu yetu ya Kilimanjaro Queens kwa kuiwakilisha vizuri Tanzania katika michuano CECAFA na kuibuka mabingwa kwa kuweza kuruka vizingiti vyote vilivyokuwepo katika muchuano hiyo” alisema Mhe. Nnauye

Serikali itaendelea kuweka nguvu ya kutosha na kuungana na timu zetu kuwasaidia kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi katika michezo mbalimbali, amesema Mhe. Nnauye.Mhe. Nnauye amesema kuwa Tanzania inaanza kuona matunda ya uwekezaji wa muda mrefu kwani haikuwa kazi raisi kwa Kilimanjaro Queens kufikia fainali na kuwa mabingwa kwa kupambana na timu ngumu na kuweza kushinda.

Aidha Mhe. Nnauye amewahaidi wachezaji wa Kirimanjaro Queens kuwaalika bungeni katika Bunge lijalo kwa ajili ya kuwapongeza na kuwaandalia mechi ya kirafiki kutambua mchango wao wa kuipeperusha bendera ya Tanzania kati yao na wabunge wanawake. Timu zilizoshiriki katika michuano ya kombe la chalenji la CECAFA ni pamoja na Tanzania, Burundi, Zanzibar, Kenya, Ethiopia, Rwanda pamoja na mwenyeji Uganda. Mashindano ya Kombe la Chalenji la CECAFA kwa timu za wanawake yamefanyika kwa mara ya kwanza jambo linaloleta tafsiri kuwa michuano hiyo inaweza kuinua soka la wanawake kwa ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati