Na Bodi ya Filamu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nnape Nnauye amesisitiza kuwa wasambazaji wote wa filamu kutoka nje lazima waingie mikataba na wazalishaji wa filamu watakazotaka kuzisambaza nchini. Kauli hiyo ya Waziri Nnape ameitoa kwenye kikao baina ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na jumuiya ya wasambazaji wa filamu kutoka nje kilichofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri Nnape amesema “kuingia mikataba na wazalishaji wa filamu ni takwa la kisheria lisiloepukika”. Aliendelea kusisitiza kwamba kazi ya serikali ni kuhakikisha inasimamia sheria hata kama sheria hizo zitakuwa haziwafurahishi walio wengi.
Kikao hicho baina ya Waziri Nnape na wasambazaji wa filamu kutoka nje ni mwendelezo wa vikao vya kurasimisha tasnia ya filamu nchini. Awali Waziri Nnape aliwaagiza watendaji wa wizara yake pamoja na taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kwa pamoja na jumuiya ya wasambazaji wa filamu kutoka nje kuunda kamati ndogo ambayo itakuwa na kazi ya kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wasambazaji wa filamu za nje na kuzitolea ufumbuzi.
Ikumbukwe mwezi Julai Waziri Nnape pamoja na Bodi ya Filamu Tanzania walifanya operesheni ya kukamata kazi bandia za wasanii. Kwenye zoezi hilo mitambo ya kudurufu kazi za wasanii na zaidi ya santuri(CD na DVD) 600,000 zilikamatwa. Baada ya zoezi hilo wasambazaji wa filamu kutoka nje kupitia jumuiya yao na mbunge wa Ilala Mussa Azzan waliomba kukutana na uongozi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Baada ya kikao kufanyika Waziri Nnape aliagiza iundwe kamati ndogo itakayoshughulikia changamoto zinazowakabili wasambazaji wa filamu za nje chini ya uenyekiti wa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania.
Kwa upande wake Mbunge wa Ilala Mussa Azzan (zungu) amewataka wasambazaji hao kuheshimu maazimio waliyoyafikia baina yao na serikali kupitia kamati ndogo iliyoundwa na Mheshimiwa Nnape.
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHESHIMIWA NAPE MOSES NNAUYE AKISISITIZA JAMBO KWENYE KIKAO NA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE. MHESHIMIWA NNAPE AMEWAASA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE KUHAKIKISHA WANAINGIA MIKATABA NA WAZALISHAJI WA FILAMU WANAZOTAKA KUZISAMBAZA HAPA NCHINI KWANI NI TAKWA LA KISHERIA LISILOEPUKIKA.
 1. MBUNGE WA ILALA MHESHIMIWA MUSSA AZZAN (ZUNGU) AKIZUNGUMZA NA WASAMBAZAJI WA FILAMU KUTOKA NJE(HAWAPO PICHANI) AMBAO WALIHUDHURIA KIKAO BAINA YA JUMUIYA YA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE NA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO. KWENYE NASAHA ZAKE MHESHIMIWA ZUNGU ALIWAASA WASAMBAZAJI WA FILAMU ZA NJE KUTEKELEZA MAAZIMIO YALIYOFIKIWA.
1. BAADHI YA WASAMBAZAJI WA FILAMU KUTOKA NJE WAKIMSIKILIZA WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO NNAPE NNAUYE WAKATI WA KIKAO CHA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WASAMBAZAJI HAO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...