Na Sheila Simba,Maelezo

Serikali meshauriwa kusimamia uwekezaji  katika sekta za kilimo,madini na viwanda ili kufikia malengo waliojiwekea ya kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

Wito huo umetolewa na Profesa Haji Semboja katika mahojiano na MAELEZO kuhusu hali ya uchumi nchini katika kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.

“Muhimu sasa Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya Madini,kilimo na viwanda na hili litasaidia kufanya nchi kuzalisha bidhaa zitakazouzwa nchini kwa wingi bila kutengemea bidhaa kutoka nje ya nchi”,alisema Prof.Semboja.

Ameeleza kuwa taarifa ya hali ya uchumi iliyotolewa na Benki Kuu nchini imeweka wazi hali ilivyo kwa sasa,na kuongeza kuwa ni kweli uchumi upo imara kutokana na taarifa zilizokusanywa na Benki  hiyo kutoka vyanzo mbali mbali.

“Ni kweli kwamba uchumi wetu upo imara na kwamba uchumi wetu unapimwa kwa kuangalia vigezo vinne ambavyo  ni pato la taifa,mfumuko wa bei,urari wa biashara na upungufu wa fedha serikalini”,alisema Prof. Semboja.

Aidha,Prof Semboja amesema kuwa serikali kwa sasa imepunguza matumizi ya fedha yasiyo ya lazima na imeongeza makusanyo ya kodi kutoka vyanzo mbalimbali.  

“Serikali haina matumizi makubwa ya fedha kwani matumizi yanendana na mapato yanayokusanywa ”,alisema Semboja
Amesema kuwa wanaolalamikia kutoonekana kwa fedha mtaani ni wale waliokuwa wanapata pesa kwa njia ambazo sio halali na hivyo kupelekea kushindwa kupata kwa sasa kutokana na udhibiti uliwekwa na Serikali katika kukusanya na kusimamia kodi kwa utaratibu halali.

Ameongeza kuwa Serikali fedha inazokusanya zinatumika kwa manufaa ya wananchi wote na sio kwa wachache waliokuwa wakijinufaisha wenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...