Waratibu wa michuano ya Rock City Marathon, wametangaza gharama na zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mchezo huo ambazo  kilele chake kinatarajiwa kuwa Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumzia zawadi hizo jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International kwa kushirikiana na mkoa wa Mwanza Bw Mathew Kasonta alisema washindi wa kwanza wa mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh.  mil 1.5/- kila mmoja, sh. 900,000/-  kwa washindi wa pili na sh. 700,000/- kwa washindi wa tatu.

Kwa upande wa mbio za Kilometa tano ambazo zitaongowa na wakuu wa mikoa ya Mwanza na Simiyu ambazo pia zitahusisha wafanyakazi kutoka makampuni mbalimbali (Corporate) pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, Kasonta alisema washindi watapatiwa zawadi za heshima kwa makampuni huku pesa zilielekwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi.

 “Washindi wa mbio za Kilometa tatu ambazo zipo mahususi kwa ajili ya wazee watapatiwa sh 50,000/- kwa washindi wa kwanza huku washindi wa pili na watatu pia watapatiwa pesa taslimu,’’ alisema Kasonta huku akiongeza kuwa kwa washindi wa mbio za kilometa 2 zitakazohusisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 watapatiwa sh 30,000 kila mmoja.

Zaidi aliongeza kwamba washindi kwanza kwenye  mbio fupi  za mita 100, 400, 800 na 1500 ambazo ni mahususi kwa wanafunzi watapatiwa zawadi y ash 50,000/ kila mmoja (wanaume na wanawake), sh 30,000 kwa washindi wa pili huku washindi watatu wakiambulia kiasi cha sh 20,000 kwa kila mmoja.

“Kubwa zaidi pia ni kuwashukuru sana wadhamini wa mbio hizi kwa kuendelea kutuunga mkono kwenye maandalizi haya yaani kampuni za Freidkin Conservation Fund na African Wildlife Trust, Benki ya NMB,  New Mwanza Hotel, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Real PR Solutions, kampuni ya Fabec, Tiper, Puma Energies, Clouds Fm, Jembe Fm, Barmedas Tv na EF Out Door alitaja.

Alitoa wito kwa washiriki zaidi kuendelea kujisajili ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo mbali na kuibua vipaji vya mchezo wa riadha hapa nchini pia zinalenga  kupambana na ujangili pamoja na kutangaza utalii katika katika Ziwa ya Ziwa.

“Kwa wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa jirani wanaweza kujisajili kwa kuchukua fomu katika vituo kadhaa vikiwemo Ofisi za michezo wilaya zote za mkoa wa Mwanza, Ofisi zote za riadha mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga,   Uwanja wa Nyamagana,  Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino  Mwanza, Kituo cha michezo  Malya, Shule ya Kimataifa ya Isamilo,  Mwanza  Hotel.


“Kwa upande wa Dar es Salaam Fomu za ushiriki pia zinapatikana katika ofisi za Kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu jengo la ATC, jijini Dar es, Salaam,” alihitimisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...