Meneja
Mradi, Ushirikishwaji wa Vijana - TYVA, Alfred Kiwuyo akiwaelezea
washiriki dhima ya kongamano la vijana waliokutana kujadili haki na
wajabu kwa vijana katika maendeleo ya Taifa. (Picha na Geofrey Adroph)
TYVA
ni asasi ya vijana ambayo imejikita na Kujipambanua kupigania jamii
yenye haki na usawa, amani na misingi ya kidemokrasia na yenye ushiriki
hai na wenye tija kwa vijana katika shughuli za maendeleo imeandaa
kongamano hili kuwawezesha vijana kujadili Haki na Wajibu kwa Vijana na
mstakabali wa Taifa kwa ujumla. Kongamano hili pia lilikuwa na dhima ya
kupanua uelewa na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli
za maendele ya Taifa kwa ujumla.
Wakili
Chikulupi Kasaka, akitoa mada ya Haki na Wajibu wa Vijana kwa vijana
mbalimbali wa vyoni na mtaani waliokuta kujadili haki na wajibu wao
katika jamii iliyofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es
salaam iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA .
Mwenyekiti
wa Bodi ya washauri ya Vijana(YAB) Femina Hip, Hassan Pukey akitoa mada
kwa vijana waliofika katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA ili kujadili haki na wajibu wa vijana na katika jamii.
Makamu
Mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumzia mchakato wa baraza la
vijana na jinsi vijana walivyoshirikishwa katika kutoa maoni ya mchakato
mzima iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA na kufanyika katika
ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam leo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...