Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya Bollore Transport and Logistics Tanzania Limited imeweka mikakati ya kuendelea kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyoo mashuleni na miundombinu ya maji katika wilaya ya Ilala.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa jina hilo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo kwa nchi za Tanzani, Rwanda na Burundi Regis Tissier amesema kuwa wameweza kushirikiana na manispaa ya wilaya ya Ilala katika ujenzi wa bomba la maji  kutoka Buguruni Mivinjeni na baada ya kuharibiwa na mvua za mwaka jana na kuwa na dalili za kutokea magonjwa ya milipuko.

Tissier amesema, kampuni ya Bollore imeweza kusaidia Shule ya Msingi Msasani kwa kuweka mradi wa gesi asilia ambapo inaweza kuja kutumika kwa matumizi ya kupika vyakula vya mashuleni na mengine pia.

Kuweza kuendelea kuleta maendeleo nchini, Ballore imeweka mikakati ya kuchukua hatua ya kuhakikisha wanasaidiana katika maendeleo katika jamii, kuajiri wafanyakazi wengi ambapo mpaka sasa asilimia 98 ni watanzania na kushirikiana na makampuni mengine katika biashara.

Ballore wana mikakati ya kuendelea kutanuka zaidi kibiashara na kuleta mirdi mipya zaidi nchini ambapo mpaka sasa wanahusika na masuala mbalimbali ikiwemouchimbaji wa nishati ya mafuta na madini, wakala wa forodha na usafirishaji wa mizigo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bollore Transport and Logistics Tanzania, Rwanda na Burundi Regis Tissier akizungumza wakati wa utambulisho wa jina jipya la kampuni hiyo jana Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bollore Transport and Logistics Tanzania, Rwanda na Burundi akiwa pamoja na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo  Branko Ng'inja (kushoto) na   Meneja mkuu wa AMI-ICD Augustin Ayishashe (Kulia).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...