THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

BENKI YA CRDB YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NCHI NZIMA

MKURUGENZI wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, amewataka wateja wa benki hiyo ndani na nje ya nchi kutumia vema fursa ya kutoa maoni ya namna ya kuboresha huduma ndani ya benki hiyo.

Mwambapa alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua wiki ya huduma kwa wateja Duniani, ambako alizinadi Akaunti mbili za Dhahabu na Thamani, ambazo zimetajwa kuwa na faida na riba kubwa kwa wateja watakaofungua na kuzitumia.

Alibainisha ya kwamba benki yake imejipanga kupokea maoni yote kutoka kwa wateja ambayo yatachakatwa na kufanyiwa kazi ili kuboresha huduma zao kwa wateja ambao ndio mhimili mkuu wa mafanikio ya CRDB.

“Maazimio yetu mwaka huu yako chini ya kauli mbiu isemayo: Tunasikiliza, Karibu, Tukuhudumie. Matarajio yetu ni kuona wateja wakiibeba na kuitumia kauli mbiu hiyo kwa ustawi wa huduma za kibenki tunazowapatia,” alisema.

Aliongeza ya kwamba, benki yake imetumia takribani miaka mitano katika kuiweka kwa vitendo kauli mbiu ya CRDB isemayo: Benki Inayomsikiliza Mteja, hivyo sasa ni wakati wa kupokea mrejesho kutoka kwa wateja juu ya wapi wanakopaswa kuboresha.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay (kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na wa pili kushoto ni Mdhibiti wa tawi la Azikiwe, Bertha Mwakibete.
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la PPF Tower, Cornell Meseyeck wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay akisalimina na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi (kulia), wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la PPF Tower, Cornell Meseyeck wa pili kulia.