Benki ya KCB Tanzania imezindua kampeni ya kutoa huduma za kibenki zisizo na foleni wala usumbufu inayoitwa JIULIZE KWANINI. Kampeni hii itawapatia wateja huduma za kibenki popote pale walipo kupitia simu za mkononi (mobile banking), mtandao wa intaneti (Internet banking) kadi za visa na huduma za kutuma na kupokea pesa papo kwa hapo sehemu yoyote Afrika Mashariki. Hii ni kuwawezesha watanzania kutumia muda wao mwingi kwenye shughuli za kujiletea maendeleo kwa kuwapunguzia foleni na usumbufu wa kwenda benki. 

“Tunaelewa kuwa shughuli za kutafuta kipato huwapeleka watanzania sehemu mbali mbali na hivyo huhitaji kupata huduma za kibenki pale walipo na kwa haraka. JIULIZE KWANINI Uhangaike kwenda mpaka benki kupata huduma hizi?” alisema Christine Manyenye, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya Umma wa benki ya KCB.

Pia Bi. Manyenye alisema kuwa kwa sasa ni benki ya KCB pekee inayotoa huduma za malipo ya papo kwa hapo kwenda popote Tanzania,Rwanda, Uganda, Burundi, Kenya, na Sudani ya Kusini. Na kwa hivyo wafanyabiashara wanaweza kununua, kulipia au kuuza bidhaa za biashara zao papo hapo. Na hivyo kuongeza maradufu mzunguko wa biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Wateja wetu wanapaswa kupata huduma za kibenki kwa haraka, usalama na bila usumbufu” alisema Bi. Manyenye. “Na hivyo tunasema JIULIZE KWANINI uendelee kuhatarisha maisha kwa kubeba pesa nyingi au kulipa kwa fedha taslimu wakati wanaweza kutumia kadi za KCB visa. Hizi huwezesha mtumiaji kutoa pesa kwenye ATM popote pale duniani, kununua vitu mtandaoni na kulipia kwenye maduka na migahawa popote duniani”.

Bi Manyenye aliendelea kwa kusema kuwa mobile banking na Internet Banking ya benki ya KCB inawawezesha watanzania kufanya malipo wakiwa manyumbani kwao, maofisini au hata safarini bila usumbufu wa kuhitaji kwenda benki. “JIULIZE KWANINI usimame muda mrefu kwenye foleni ya benki au vituo vya kulipia mahitaji yako kama luku, ving’amuzi vya televisheni au huduma za maji wakati ukiwa na mobile banking na Internet Banking ya benki ya KCB unaweza kufanya hayo yote popote pale utakapokuwa?” .
Akamalizia kwa kuwataka wananchi ambao bado hawajajiunga na benki ya KCB kujiunga leo na kupata huduma za kibenki zisizo na usumbufu wa foleni. 
 Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya Umma, Christine Manyenye (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusiana na kampeni ya JIULIZE KWANINI. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Barry Chale (Katikati) na Mkuu wa uendeshaji na teknohama Rojas Mdoe (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Barry Chale (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya JIULIZE KWANINI. Pamoja nae ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya Umma, Christine Manyenye (Katikati) na Mkuu wa rasilimali watu Joyce Wiki Mwashigadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...