Na Rhoda Ezekiel -Globu ya Jamii Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ameipongeza idara ya Afya Wilayani Kakonko kwa jitihada ya kupungua kwa vifo vya mama na mtoto kutoka vifo 404 Kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka kutokana na wadau wa Afya kuchangia Huduma hiyo kww ushiriki wa pamoja na watumishi wa idara ya afya.

Kauli hiyo imetolewa wakati mkuu huyo akipokea msaada wa vitanda Na magodoro 18 kutoka katika kampuni ya taasisi za kifedha NMB Kanda ya magraribi Tabora tawi la Kakonko lengo likiwa ni kuchangia kupunguza vifo vya mama Na Mtoto katika wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma.

Ndagala alisema jitihada zinazofanywa na wadau pamoja na idara ya afya zinaonyesha wazi kuwa vifo hivyo vitazidi kupunguza siku hadi siku.Licha ya kuwepo jitiada za kufikia malengo hayo sekta ya afya bado inakabiliwa matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na madawa vifaa tiba na miundo mbinu hatua inayoilazimu serikali Taasisi na wadau mbambali kujitoa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliipongeza Benk hiyo kwa msaada ulioutoa katika hospital ya wilaya na kuwaomba watumishi na wananchi kuvilinda vitanda Na magodoro yaliyotolewa ilikuwezakusaidia Wananchi Na Serikali kwa ujumla ilikuweza kupunguza kabisa ya ukosefu wa vitanda.

Nae Meneja wa benki ya NMB tawi la Kakonko,Leonard Mgaya alisema benk hiyo imeamua kuboresha mazingira ya kujifugulia kwa wanawake ilikupunguza vifovitokanavyo na Huduma mbovu zinazotolewa katika vituo vya Afya Benki hiyo imetoa msahada wa Vitanda na Magodoro 18 yenye thaman ya tsh milion kumi katika kituo cha Afya Kakonko kinachotumika kama hospitali ya wilaya ambapo msahada wa awamu ya kwanza vitanda 9 ulitolewa mwezi tisa .

Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya kakonko Joseph Tutuba amesema katika wilaya yake vifo vya wanawake wajawazito vimepungua kwa chini ya wastani ya vifo 404 kati ya 100,000 hali ambayo ni chini ya zaidi wastani wa kitaifa ambao ni 432 kwa vizazi hai na kudai kuwa hatu hiyo ni kutokana na kutumia ipasavyo michango inayotolewa na wadau wa afya.

Nae Emakulata Lusinge ambae ni muuguzi mkuu katika wodi ya wanawake ameeleza kuwa hapo awali katika kituo hicho, walikuwa wanapata shida sana katika kuwahudumia wagonjwa kwani kutokana na uhaba wa vitanda wagonjwa wamekuwa wakilala watatu na wengine kulala chini hali ambayo ni hatari kwa afya za wagonjwa hasa watoto wachanga.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani),mapema leo wakati alipokuwa akipokea msaada wa vitanda na magodoro 18 kutoka katika kampuni ya taasisi za kifedha NMB Kanda ya magharibi Tabora tawi la Kakonko, lengo likiwa ni kuchangia kupunguza vifo vya mama na Mtoto katika wilaya ya Kakonko Mkoani wa Kigoma.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akipokea msaada wa vitanda na magodoro 18 kutoka kwa Meneja wa benki ya NMB tawi la Kakonko,Leonard Mgaya.Lengo msaada huo ni kuchangia kupunguza vifo vya mama na Mtoto katika wilaya ya Kakonko Mkoani wa Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...