Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la michezo Tanzania (BMT) limetangaza kutoutambua Mkataba wa ukodishwaji wa klabu ya Yanga kwa kuwa ni kinyume na katiba ya klabu hiyo.

Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa mkataba huo kati ya Baraza la Wadhamini wa Yanga na kampuni iliyoikodi klabu hiyo, haukufuata taratibu.

"Ili Yanga iweze kubadili jina na kuitwa Yanga Yetu ni lazima ipite kwa msajili. Wao hawajaenda kwa msajili wanaanza kutangaza jina jipya. Huko ni kupinga katiba," amesema Kiganja.

Baraza limeagiza klabu kutunia vikao mbalimbali vinavyotambulika kikatiba na viitishwe kuzingatia kanuni na taratibu ambapo kamati ya utendaji inatakuwa kukaa na kujadili jambo hilo kama lina faida au hasara.

Na wakishamaliza kulijadili waandike muhtasari na kuupeleka katika ngazi ya juu ya klabu waliangalie na baadae kufanya mabadiliko ya katiba na kisha kuisajili ili kuweza kuingia kwenye mfumo mpya.

Kiganja amesema kuwa kutokana na utaratibu walioutumia Yanga hautambuliki na hawataza kutambua mabadiliko hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...