Na Mwandishi wetu.
BODI ya Filamu Tanzania leo imemkabidhi cheti na hundi yenye thamani ya shilingi Laki Mbili mwanafunzi Omary Maganga aliyefanya vizuri kwenye masomo ya filamu na runinga kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA).

Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ofisi za bodi hiyo ambapo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Abuu Kimario alimkabidhi cheti hicho na hundi kwa niaba ya Katibu Mtendaji Joyce fisoo.

Baada ya kukabidhiwa zawadi zake bwana Maganga aliishukuru Bodi hiyo ya filamu kwa kutambua juhudi za wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao. Pia ameziasa taasisi zingine za Serikali na zisizo za kiserikali kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwani kwa kufanya hivyo kunaongeza morali na ushindani.

Wakati huo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Abuu Kimario kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa bodi hiyo ametoa ahadi ya kuendelea kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yenye uhusiano na tasnia ya filamu. 

Kwa sasa Bodi ya Filamu Tanzania iko kwenye utekelezaji wa programu ya kutambua na kukuza vipaji vya wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya tasnia ya filamu nchini. Program hii ilianzishwa ikiwa na lengo la kukuza ubora wa filamu za Kitanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera kijana... Tunahitaji mabadiliko katika filamu zetu, tunawaamini kwa pamoja mtaweza.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana kaka Maganga, dah safi aisee nakumbuka jitihada zako wakt tupo sote Hostel,keep moving nakumbuka dream yako ya kutaka kuwa James Cameron Director mkubwa Duniani kila kitu kinawezekana jitihada tuu kaka
    Hongera sana tupo pamoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...