Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe (78.2KG) akitangazwa mshindi mara baada ya kumpiga kwa 'KnockOut' Bondia Chengbo Zheng (77.9KG) kutoka nchini China katika raundi kwanza kabisa ya mpambano wao usiokuwa wa Ubingwa uliomalizika usiku huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akimsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng kutoka nchini China na kupelekea mpambano huo kuisha ndani ya dakika mbili na sekunde kadhaa kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam.
Bondia Abdallah  Pazi a.k.a Dullah Mbabe akiendelea kumsukumia makonde mazito Bondia Chengbo Zheng yaliyompelekea kwenda chini na kuomba kutoendelea na mpambani huo.
Katika mambano ya utangulizi, kulikuwa na pambano hili la raundi nane lililokuwa na mvuto wa aina yake lililowakutanisha mabondia Said Mbelwa (nyeupe) na Shaban Kaoneka. hili lilikuwa na pambano la rusha nirushe, ambapo Bondia Said Mbelwa alifanikiwa kushinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi dakika ya saba ya mpambano huo.
Bondia Paul Kamata (nyeupe) akimsukumia makonde mithili ya mvua Bondia Buta Obed katika mpambano wao usio na ubingwa wa raundi nani, ulichezwa usiku wa leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es salaam. Bondia Paul Kamata alishinda kwa 'KnockOut' ya kiufundi, katika raundi ya tano ya mchezo hio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...