Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii
MAHAKAMA Kuu Tanzania, Divisheni ya Ardhi, jijini Dar es salaam imetupilia mbali maombi ya Kampuni ya Mbowe Hotels Limited inayomilikiwa na Mwenyekiti Taifa wa Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe ya kutaka kurudishwa kwenye jengo la Billicanas kwa sababu waliondolewa katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Jaji Sivangilwa Mwangesi alisema shirika hilo lilifuata taratibu zote kumwondoa mlalamikaji katika jengo hilo na kwamba inashikilia mali zake kihalali hadi atakapolipa kodi ya Sh.Bilioni 1.3  anavyodaiwa na NHC.
Akisoma uamuzi huo mapema leo Jaji Mwangesi baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, mahakama yake iliamua kutupilia mbali maombi hayo yaliyofunguliwa chini ya hati ya dharula bila kulipwa gharama.

Jaji alisema madai ya mlalamikaji kwamba aliondolewa kinyume cha sheria katika jengo hilo na kampuni ya udalali isiyosajiliwa hayana mashiko kisheria na kwamba mahakama inafutilia mbali kesi hiyo.

“Mahakama hii baada ya kupitia hoja za pande zote mbili imeona kwamba mlalamikiwa wa kwanza NHC alifuata taratibu zote kumtoa mlalamikaji katika jengo hilo.  Pia imeona kwamba kampuni ya udalali  ya Foster Auctioneers and General Traders ilifanya kazi ya kuondoa mali zake kihali, hivyo mahakama inatupilia maombi haya bila kulipwa gharama ya kesi hii” alisema Jaji Mwangesi.
Akifafanua zaidi Jaji  Mwangesi alisema pamoja na madai ya kuwepo kwa mkataba kati ya NHC na Mbowe, mkataba huo haukuwahi kutekelezwa kwa hiyo ni sawa na kwamba haupo. 
Upande wa mlalamikaji uliongozwa na Mawakili Peter Kibatala akisaidiana na John Mallya. Upande wa walalamikaji uliongozwa na Mawakili Aloyce Sekule, Aliko Mwamanenge na Mariam Mungula.
Wakili Mwamanenge akizungumza na Globu  ya Jamii nje ya viunga vya mahakama hiyo, alisema mlalamikaji alisema mahakama imetenda haki na kwamba mlalamikaji alidai kuwa na mkataba kati yake na NHC, lakini mahakama hiyo imeona mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

“Mahakama imeona dalali alifanya kazi yake kwa kufuata taratibu za kisheria na hata hizo mali zinashikiliwa na mteja kihalali hadi atakapolipa deni la Sh. Bilini 1.3 ndipo atarejeshewa mali hizo” alisema wakili Mwamanenge.
Kwa upande wake Wakili Mallya alisema wamewasilisha maombi ya kuomba nakala ya uamuzi ili waombe marejeo Mahakama ya Rufani Tanzania.

Wakili wa NHC Aliko Mwamnenge akizungumza na waandishi habari baada ya kutoka katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikihusu maombi ya Mbowe hotels kurejea katika ofisi zake,ambapo hukumu yake imetolewa leo katika  mahakama kuu kitengo cha Ardhi,jijini Dar.
 Wakili wa Mbowe Hotels, John Mallya, akizungumza na waandishi wa habari juu ya hukumu iliyotelewa na Mahakama kuhusiana na maombi ya kurejea Mbowe hotels na Mali zake,  katika mahakama kuu kitengo cha ardhi leo jijini Dar es salaam.
 Mawakili wakitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa. 
Mawakili wa Mbowe Hotels John Mallya (kushoto) na Peter Kibatala (kulia) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...