Mkurugenzi wa Sayansi AMP, Dr. Bradford Gessner akizungumza wakati wa Mkutano wa Kanda ya Afrika wa Magonjwa yatokanayo na Pneumococcal kwaajili ya Kuangalia mafanikio katika miaka 5 tangu kutambulishwa kwa chanjo ya PCV13 na kujadiliana mustakabali wa miaka mitano ijayo mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dafrossa Lyimo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya Mkutano wa Kanda ya Afrika wa Magonjwa yatokanayo na Pneumococcal kwaajili ya Kuangalia mafanikio katika miaka 5 tangu kutambulishwa kwa chanjo ya PCV13 na kujadiliana mustakabali wa miaka mitano ijayo.
Amesema kuwa Wataalamu wa chanjo ya Nimonia wamekaa na kutoa tathmni ya maradhi ya nimonia pamoja na maradhi ya mtindio wa ubongo kuwa yamepungua kutoka na kutoa chanjo kwa watoto mara baada ya kuzaliwa wakiwa na umri wa wiki 6, 10 na 14.

Amesema kuwa Lengo kuu la mkutano huu ni kutoa taarifa za karibuni za kisayansi kuhusiana na magonjwa ya pneumococcal na athari ya chanjo hiyo.
Baadhi ya wadau wa afya wakiwa kwenye mkutano wenye Lengo kuu la mkutano huu ni kutoa taarifa za karibuni za kisayansi kuhusiana na magonjwa ya pneumococcal na athari ya chanjo  jijini Dar es Salaam leo. 

 TAARIFA kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kiasi cha watu milioni 1.6 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa jamii ya pneumococcal (ambayo ni pamoja na nimonia/ homa za mapafu, homa ya uti wa mgongo na maambukizi ya damu), Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sayansi AMP, Dr. Bradford Gessner wakati wa  Mkutano wa Afrika wa magonjwa ya pneumococcal ulio kusanya viongozi na wasimamizi katika sekta ya chanjo kutoka katika nchi ambazo zimeshatambulisha chanjo au zinazotaka kutambulisha chanjo jijini Dar es Salaam leo. “Kuwepo kwa taarifa za karibuni na pia kubadilishana mafunzo ya mipango ya chanjo itawezesha washiriki kusaidia maamuzi ya nchi kwa kutumia vithibitisho.” 

“Lengo la msingi la Gavi ni kupunguza maradhi na vifo kwa watoto wachanga kupitia chanjo na Pfizer inajivunia kuwa mshirika ikijumuika na washirika wengine katika magonjwa ya pneumococcal kupitia soko la awali la kujitolea ambalo linategemewa kuweza kuepusha magonjwa haya kwa watoto milioni moja kufikia mwaka 2020,” alisema Heather Sings Mkurugenzi wa Chanjo katika Idara ya Matibabu ya Pfizer.

Tangu Gavi ilipoanza kusapoti chanjo ya PCV13 mwaka 2010, nchi 18 kutoka Africa wametambulisha chanjo hii katika mipango yao ya chanjo na kinga. Kama jina lake lilivyo PCV13 inatoa kinga dhidi ya vimelea 13 vinavyosababisha magonjwa ya pneumococcal. 

Wakati kinga inajulikana kama njia yenye mafanikio na ya gharama nafuu katika kulinda afya, magonjwa yatokanayo na pneumococcal bado yamekuwa ni tatizo kubwa katika sekta ya afya katika nchi za Afrika kusini ya Sahara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...