THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Chifu Musomba wa Bundali ampongeza Rais Magufuli

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii-ILEJE

KIONGOZI wa machifu wa kindali Wilayani Ileje , Chifu Etisoni Musomba amempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa utendaji wake tangu alipochaguliwa kuongoza taifa hili.

Chief Musomba amesema hayo katika mahojiano maalum na Globu ya jamii juu ya namna gani utawala wa jadi unavyoona mwenendo wa serikali.

“Kiukweli kwa sasa hali ni nzuri maana kumekuwa na heshima ya kutosha hata watumishi wa serikali huku vijijini tumewaona wakifanya kazi kwa bidii kutokana na kuogopa kufukuzwa tofauti na awali ambapo walikuwa wanafanya wanavyotaka na machifu tulipokemea tulidharauriwa” amesema Chief Musomba.

Chief Musomba ameongeza kuwa vijiji vimekuwa  na amani sana,watoto wanapata elimu bure na wazazi hawasumbuliwi kuhusu fedha za ada wala michango mengine iliyokuwa kero kwao.

Amesema kuwa hapo awali wazazi walilazimika kuuza mifugo yao na kuingia katika umaskini mkubwa kutokana na kulipia Ada za watoto wao pindi wanapochaguliwa kwenda Sekondari bali kwa sasa fedha kidogo wanazopata kutokana na uuzaji wa mazo zinawatosha kujikimu katika kutatu matatizo ya watoto wa shule.