Msanii Snura Mushi 'Snura'akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha Video yake ya wimbo wa  chura mara baada ya kufunguliwa wimbo huo kupigwa na kuoneshwa kwenye vituo vya Luninga pamoja na wimbo wa chura kuanza kupigwa katika vituo vya Redio hapa nchini.
 Msemaji wa 'Snura', kulia akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar e Salaam leo mara baada ya kukamilisha video mpya ya wimbo wa chura wa Snura na wimbo huo kuanza kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya Luninga pamoja na wimbo wa chura kuaza kupigwa kwenye vituo vya Redio.
Picha na Aviala Kakingo, Globu ya Jamii.

VIDEO mpya ya wimbo wa Msanii, Snura Mushi 'Snura' wa Chura ambao ulikuwa umefungiwa na Serikali, wimbo  huo umefunguliwa na kuanza kuchezwa na kuoneshwa kwenye vituo vya Luninga pamoja na kupigwa kwenye vituo vya Redio.

Hayo yamesemwa na Msanii, Snura Mushi wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wimbo huo ameurekodia Video mpya yenye maadili ya Kitanzania na yenye staa zote na inaelezea maana halisi ya chura kama alivyomaanisha kwenye utunzi wa wimbo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CHURA UMEFUNGULIWA:

    Chura huru maachiwa, uruke anavyotaka,
    Chura usijetibuwa, idharani sijefika,
    Ruka kwa unavyojuwa, heshima na hadhiyo weka,
    Chura mwanzo litibuwa, 'rumande' wakakuweka.

    Kwenye mito na mabwawa, rukhusa kuruka ruka,
    Bahari hujazuiwa, piga mbizi ukitaka,
    Huna cha kubughudhiwa, mwanzo livuka mipaka.
    Chura sasa umekuwa, pole yote lokufika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...