Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Geita 

Shirika la Misaada na Maendeleo ya Jamii (CODERT) limejipanga kuwasaidia jumla ya wananchi 7000 wanaoishi katika mazingira magumu Mkoani Geita ili waweze kujikwamua kutoka katika lindi la umasikini linalowakabili. 

Shirika hilo ni moja ya mashirika yanayoshirikiana na Shirika la Plan International katika kutekeleza Mradi wa Uondoaji Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) na kuratibiwa na shirika la plan International kwa kuwapatia wananchi hao vifaa pamoja na elimu ya ujasiriamali.

Hayo yamesemwa leo Mkoani Geita na Msimamizi wa Miradi wa shirika hilo, Edward Saramba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu njia wanazozitumia kuwainua wazazi na vijana wa mkoa huo ili waache kuwapeleka watoto walio na umri chini ya miaka 18 kufanya kazi katika maeneo ya migodi.

Saramba amesema kuwa mradi huo unaoratibiwa na shirika la Plan International umewasaidia wananchi wa mkoani Geita kuinua maisha yao kwa kuwasaidia kuunda vikundi vya kuweka na kukopa pamoja na kuwapatia vifaa mbalimbali vinavyowawezesha kujipatia vipato ambavyo vinawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku. 
Mmoja wa wananchi waliosaidiwa kupata mradi wa kuku kupitia Mradi wa Uondoaji wa Ajira Hatarishi na Vitendo vya Ukatili kwa Watoto unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), unaratibiwa na Shirika la Plan International na kutekelezwa katika Wilaya 3 za Mkoa wa Geita, Shabani Masanja akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi huo ulivyomsaidia. 
Msimamizi wa Miradi wa Shirika la Misaada na Maendeleo ya Jamii (CODERT), Edward Saramba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu njia wanazozitumia kuwainua wazazi na vijana wa Mkoa wa Geita ili waache kuwapeleka watoto walio na umri chini ya miaka 18 kufanya kazi katika maeneo ya migodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...