Meneja masoko wa Benki ya CRDB Fredrick Siwale akizungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja mjini Babati Mkoani Manyara, katikati ni Mkurugenzi wa mji huo Fortunatus Fwema na Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald Paul.
Meneja wa utawala wa Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Domitila Bugomola, akizungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja.

………………………………………………

Benki ya CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, imefanikiwa kutoa mikopo ya sh16.1 bilioni kwa wajasiriamali, watumishi wa Serikali, watumishi wa sekta binafsi, vyama vya kuweka na kukopa na asasi za fedha.

Watumishi wa serikali na wasekta binafsi 1,604 walikopeshwa sh12.8 bilioni na wajasiriamali 84 walikopa sh3.3 bilioni ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara na wakulima.Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Babati, Ronald Paul akizungumza kwenye kilele cha wiki ya huduma kwa wateja, alisema wamedhamiria kuwapa wateja wao huduma bora na kuwanyanyua kiuchumi.

Paul alisema kwa muda wa miaka miwili tangu waanzishe huduma ya benki hiyo mkoani Manyara, wamefanikiwa kufungua matawi mengine madogo wilaya za Mbulu, Hanang, Simanjiro na Kiteto.Alisema pia wamefanikiwa kufungua huduma za matawi madogo yaliyopo Magugu, Haydom na Mirerani ambayo kupitia hayo wameweza kupata akaunti za halmashauri za wilaya.

Alisema kwenye matawi yao madogo wamefanikiwa kuwa na huduma za ATM ambazo wamefungua 10 kwenye mkoa huo na zinafanya kazi kwa muda wa saa 24.“Kwa kipindi hiki tumefanikiwa kuongeza ajira kwa watanzania hususani kwa wana Manyara kutoka wafanyakazi 12 hadi 37 kutokana na matawi mengine madogo yaliyofunguliwa katika wilaya mbalimbali,” alisema.

Alisema wamefanikiwa kupata amana za sh11 bilioni zilizotokana na wateja 12,000 waliofungua akaunti za akiba, watoto jumbo, akaunti za malkia, akaunti maalum, bidhaa nyingi za kibenki za Simbanking, ATM na fahari huduma.Mkurugenzi wa mji wa Babati Fortunatus Fwema alitoa wito kwa benki hiyo kuwatafutia wateja wa mbaazi wa nje ya nchi kwani hivi sasa wakulima wengi wanapata changamoto ya soko la zao hilo.

Fwema alisema kutokana na benki hiyo kutoa huduma za fedha hadi nje ya nchi hasa nchini India, wangetumia fursa hiyo kwa kuwaunganisha wakulima hao moja kwa moja na soko la mbaazi ambalo wanunuzi wengi hutoka nchini India.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...