Na Ally Daud-Maelezo

DAWA bandia na yasiyo sahihi kwa matumizi ya binadamu yamekamatwa maeneo ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini baada ya kufanyika ukaguzi maalum wa kutafuta dawa bandia katika maeneo hayo iliyofanyika hivi karibuni.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakati wa kutoa Matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa uliofanyika katika mikoa ya Kanda za Ziwa na Nyanda za Juu Kusini.“Kutokana na ukaguzi maalum tulioufanya katika Kanda za Ziwa pamoja na Nyanda za Juu Kusini wa kutafuta dawa bandia na zisizo sahihi kwa matumizi ya binadamu tumefanikiwa kukamata dawa bandia za aina tano ambazo zipo kwenye makundi mawili ya Dawa za malaria na Viua vijasumu(Antibiotics)” alisema Bw. Sillo.

Aidha Bw. Sillo amesema kuwa ukaguzi huo maalum umeweza kusaidia kukamata dawa ya malaria aina ya vidonge vya Quinine ambayo inadaiwa kutengenezwa katika kiwanda cha Elys Chemical nchini Kenya na nyingine zinatengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha Shelys Phamaceuticals Ltd.Mbali na hayo Bw. Sillo amesema kuwa pamoja na kukamata dawa bandia pia zoezi hilo lilifanikiwa kubaini na kukamata dawa zilizoisha muda wa matumizi , zisizosajiliwa na zenye ubora duni zenye thamani ya Tsh. Milioni 17.463.

Bw. Sillo ameongeza kuwa Ukaguzi huo ulitokana na kuwa na taarifa za awali ambazo zilionyesha uwepo wa dawa bandia katika maeneo ya Geita na Mara mwezi Agosti na Septemba mwaka huu na kusistiza kwamba zoezi hilo la ukaguzi linaendelea nchini kote na watakaokutwa na hatia watachukuliwa hatua stahiki.Kwa upande wa Msajili wa Baraza la famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe amesema kuwa wataalamu wa madawa watakaokutwa na hatia ya kusambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi.

“Wataalamu wa dawa ambao wanasambaza na kuhudumia dawa bandia watafutiwa usajili na kuacha kutoa huduma kwa mujibu wa sheria ya dawa , chakula na vipodozi pindi watapogundulika” alisema Bi. Shekalaghe.Zoezi hilo la Ukaguzi maalum wa dawa bandia ulianza Oktoba 4 mwaka huu linafanywa kwa ushirikiano wa TFDA, Jeshi la polisi pamoja na Maafisa kutoka Baraza la Famasi litakuwa endelevu ili kuhakikisha dawa bandia zinatoweka nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akionyesha baadhi ya dawa bandia zilizokamatwa baada ya ukaguzi maalum uliofanyika maeneo ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini wakati alipoongea na waandishi wa habari katika mkutano wa kutoa matokeo ya ukaguzi wa dawa bandia huo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo katikati akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa mkutano wa kutoa matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa bandia uliofanyika maeneo ya Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini , wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa dawa na bidhaa Nyongeza Bw. Adonis Bitegeko na kushoto ni Msajili wa Baraza la famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo katika akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa dawa na bidhaa Nyongeza Bw. Adonis Bitegeko kulia na Msajili wa Baraza la famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe kushoto wakionyesha baadhi ya dawa bandia wakati wa mkutano wa kutoa matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa bandia uliofanyika jijini Dar es salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo hayupo pichani wakati wa mkutano wa kutoa matokeo ya ukaguzi maalum wa dawa bandia uliofanyika jijini Dar es salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...