THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DAWASCO NA DAWASA SHIRIKIANENI KUONDOA KERO YA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM-MHADISI MBOGO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati amezindua Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) iliyofanyika mjini Bagamoyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Mfutakamba amezitaka taasisi hizo kuongeza ushirikiano,haswa kwa wafanyakazi kwa kuwaandalia semina za mafunzo kwa pamoja ili waweze kufahamiana na kushirikiana kwa pamoja katika kuondoa kero ya Maji iliyopo jijini Dar es salaam.

“Mimi faraja yangu ni kuona DAWASCO na DAWASA mnashirikiana haswa wafanyakazi kwa kuwa kitu kimoja katika kutimiza majukumu yao, muone tatizo la Maji ni lenu wote ,naamini mkipendana na kuwa wamoja mtasaidia sana kuondoa kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam” alisema Mfutakamba.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu amemshukuru katibu mkuu kwa kufika na kuzindua semina hiyo na pia amewataka washiriki hao kutumia elimu watakayopata kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na kutatua kero ya Maji kwa jiji la Dar es salaam.

“Kwa niaba ya DAWASCO na DAWASA tunakushukuru katibu mkuu kwa kuweza kushiriki nasi kuzindua semina hii ya mafunzo kwa wafanyakazi wa taasisi hizi mbili tunaona upo pamoja nasi hivyo na mimi napenda kuwa sisitizia washiriki wa semina hii kutumia elimu na ujuzi watakaopata kuboresha huduma ya Maji kwa kuwa wabunifu kwenye maeneo yao ya kazi nakuondoa kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa pwani” alisema Kitundu.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza katika uzinduzi wa Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) Mkoani Pwani 
 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu akizungumz machche kwenye uzinduzi wa Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) Mkoani Pwani 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu wakiwa kwenye picha ya pamoja na DAWASCO na DAWASA Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii