NA VICTOR MASANGU

MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo Mohamed Mwanga amesema kuwa atahakikisha anazisimamia  na kuzivalia njunga ipasavyo fedha  amabzo zinazotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuweza kuwasadia vijana na wakinamama lengo ikiwa ni kuona zinatumika katika vikundi mbali lli  kuweza kukuza uchumi na kuleta chachu ya kimaendeleo.
Mwanga ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha redio cha Jijini Dar es Salaam kuhusina na changamoto  mbali mbali zilizopo katika utendaji wa kazi pamoja na mikakati kabambe  aliyoiweka katika kuwahudumia wananchi wake wa Bagamoyo.
Alisema kwamba halmashauri zinanapaswa kutenga kiasi cha asilimia kumi cha makusanyo ya mapato yake ambapo vijana wanatakiwa kupatiwa asilimia tano na kwa upande wa wakinaamama wanatakiwa wapatiwe asilimia tano kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

“Mimi kama mkuuwa Wilaya ya Bagamoyo mikakati yangi ni kuhakikisha kwamba fedha hizo ambazo ni asilimia kumi zinawafikia walengwa wote bila ya kuwa na ubaguzi, hivyuo nitazisimamia na kuona ni jinsi gani zinaweza kuleta mabadiliko chanya kwa vijana pamoja na wakinamama ambao watapatiwa fedha hizo,”alisema Mwanga.

Aidha mkuu huyo alisema kwamba ana imani kwamba eendapo halmashauri ikilitilia mkazo suala hilo la kuhakikisha kiais hicho cha asilimia kumi kinatolewa katika kila bajeti kutaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa kuviwezesha vikundi vya aina mbali mbali ili viweze kuendesha biashara zao na kukuza mitaji waliyonayo.
Pia alifafanua kuwa fedha hizo zinatolewa kwa uataratibu maalumu ambapo inatakiwa vijana au wakinamama kuunda vikundi vyao na kuvisajili ili pindi fedha hizo zinapotolewa ziweze kuwafikia walengwa kwa wakati na kuweza kuwanufaisha kwa kiais  kikubwa katika kuendeleza biashara zao ambazo wanakuwa wanazifanya ziweze kukua zaidi.
 “Katika Wilaya yangu ya Bagamoyo kwa sasa nina halmashauri mbili, ambapo kuna halshauri ya bagamoyo, pamoja na halmashauri ya mji mdogo chalinze, kwa hivyo zote hizi zinatakiwa kutenga asilimi hiyo kumi kwa ajili ya kuviwezesha vikundi hivyo nbila ya kuwa na upendeleo wa aiana yoyote,”aliongeza Mwanga.
Alisema kwamba kwa sasa kuna fedha ambazo tayari zimeshatolewa na halmashauri  kwa ajii ya kuvisaidia vikundi hivyo vya wakinamama na vijana, ambapo katika halmashauri ya bagamoyo kumeshatolewa kiasi cha shilingi milioni 120 na kuongeza kuwa fedha hizo zitakuwa zinatolewa kwa mzunguko ii ziweze kuwafikia walengwe wote.

Katika hatua nyingine Mwanga alitoa wito kwa vijana na wakinamama ambao watapata fursa ya kupatiwa fedha hizo kuhakikisha kuwa  wanazitumia vizuri katika kuendeshea biashara zao ili kuweza kukuza mitaji yao na kuondokana na kuwa tegemezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...