Mkuu huyo wa Wilaya ya Chemba ameyasema hayo leo wakati wakiaga mwili wa Mke wa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kelema Balai aliyeuawa kwa kupigwa mshale wa sumu na kijana ambaye mpaka sasa ametoweka hapo kijijini kutokana na ugomvi ambao umedumu kwa muda mrefu kati ya mume wa marehemu na kijana huyo anayehisiwa kutenda unyama huu. 


Imesemekana mtuhumiwa akiwa na wenzake wawili siku ya tukio majira ya saa mbili na nusu usiku walivamia nyumbani kwa marehemu na kuanza kumshambulia kwa fimbo mume wa marehemu na kukimbizwa hospital ya jirani kabla muhisiwa hajarejea na kutekeleza unyama huo.
Mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Polisi ambao ni baba wa kijana huyo kwa kuwa alishiriki katika tukio la awali la kumjeruhi Mwalimu  Manyama kwa kushirikiana na kijana wake kumjeruhi kwa fimbo. (Mwl Manyama ndiye mume wa marehemu)

Watu wengine ni Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na Mtendaji wa Kijiji. Hawa wanashikiliwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya baada ya maelezo yao waliyoyatoa kuhusiana na namna walivyoshughulikia tukio hili kuanzia usiku mpaka asubuhi kuto mridhisha Mkuu wa Wilaya. Kwani toka usiku wa tarehe 3 mpaka saa tatu wahisiwa walikuwepo kijijini kabla ya kutoweka na Viongozi hao hwakuwa wamechukua hatua zozote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...