THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DC HANDENI,MH GONDWE AKUTANA NA WATENDAJI WA WILAYA NGAZI MBALIMBALI,AWATAKA KUSIMAMIA MISINGI YA UTAWALA BORA NA KUHUDUMIA WANANCHI

Na Alda Sadango-Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Handeni
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amewataka Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti wa Vijiji kusimamia misingi ya utawala bora katika kutimiza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi. Mh Gondwe aliyazungumza hayo katika kikao kazi alichokiitisha mwishoni mwa iki Oktoba 28/2016. 

Mh. Gondwe amewataka viongozi kusimamia rasilimali za umma ikiwemo misitu, ardhi na usimamizi wa suala zima la usafi na mazingira katika maeneo yao. Pia aliwakumbusha kusikiliza kero za wananchi kuanzia ngazi ya chini ikiwa na kushughulikia malalamiko yao kabla ya kufika ngazi ya Wilaya. Wananchi wanatakiwa kusikilizwa matatizo yao, pale ambapo ngazi za chini zimeshindwa basi ngazi ya Wilaya itashughulika kikamilifu.

Mh. Gondwe amewaeleza Maafisa Watendaji na wenyeviti wa Vijiji kwamba kutokana na hali mbaya ya chakula suala la kulima ekari moja ya muhogo kwa kila kaya ni lazima sio jambo la hiari tena. Aidha amepiga marufuku kutumia mazao ya chakula katika kutengenezea pombe kwa sababu hali ya chakula kwa sasa katika Wilaya ya Handeni sio nzuri.” Ni marufuku mazao ya chakula kutumika katika kupikia pombe kwa sababu hatuna chakula cha kutosha” alisema.

Ametoa tahadhari kwa viongozi na Watendaji kuwa makini na taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s)zinapokuja kufanya huduma katika maeneo yetu, kwani taasisi nyingine zinakuwa hazina dhamira njema kwa wananchi kwani zimeonekana kufanya mambo ya kitapeli mfano baadhi yao zimekuwa zikichangisha fedha kwa wananchi bila kufuata utaratibu., ,”Viongozi wote na Maafisa Tarafa pale mnapoona kwenye maeneo yenu kuna taasisi zisizo za kiserikali zimekuja na hamuelewi mienendo yao tafadhali naomba mtoe taarifa mapema ili Uongozi wa Wilaya uweze kushughulikia mapema ” alisema.
 Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa.
 Hapo ni mkurugenzi mtendaji akizungumza na viongozi watendaji na Maafisa Tarafa. 
 Mmoja wa Wenyeviti wa Vijiji akizungumza katika kikao kazi hicho.
 Afisa utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Abel Noel akitoa ufafanuzi wa misingi ya Utawala bora.
 Viongozi watendaji, Maafisa Tarafa waliofika katika kikao kazi cha DC.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA