THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DC ILALA AGOMA KUPOKEA RIPOTI YA SOKO LA SAMAKI FERRY

Na Humphrey Shao,Dar es Salaam .

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, amegoma kupokea ripoti ya soko la Samaki Ferry kutoka kwa Meneja wa soko hilo,baada ya kubainika ''MADUDU'' yaliyomo ndani ya ripoti hiyo. 

DC Mjema aliamua kufanya hivyo mara baada ya kubaini kuwa makusanyo ya ushuru yaliyomo ndani ya ripoti hiyo ni ya udanganyifu na kwamba mifumo ya uendeshaji iliyopo ndani soko hilo ni dhaifu na haikidhi viwango vya ubora,jambo ambalo linaishushia hadhi soko hilo ambalo ni maarufu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kusini mwa Jangwa la Sahara.
 
"Katika soko hili lazima mmfanye mpango mpya wa kuhakikisha mnaongeza makusanyo ya ushuru kutoka milioni tatu kwa siku na ziadi ili kuhimili huduma zinazohitajika kutolewa kwa wadau wa soko"amesema Mjema. 

Mjema aliagiza kuwa ndani ya miezi mitatu lazima bodi na uongozi wa Soko hilo kuhakikisha wanajenga matundu ya vyoo Ishirini tofauti na sasa ambapo kuna matundu mawili tu, ambayo yanahudumia watu zaidi ya 4000 katika soko hilo.Pia aliweka wazi kuwa bodi ya soko hilo ina mzigo mzito wa kuhakikisha soko hilo linarudi katika mstari kama lilivyo kabidhiwa na serikali ya Japan kwa Tanzania.  

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua sehemu ya soko akiwa ameambatana na Naibu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema akiangalia moja ya Chemba ya maji taka ambayo haina mfuniko wakati kwenye ripoti inaonyesha kuwa chemba hizo zina mifuniko.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akizungumza na mmoja wa wachuuzi wa Samaki katika soko la Samaki Ferry.