Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii, Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amewaasa wakulima wa Bonde la Mto Katengela Kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko kulima mazao yao kwa misimu miwili ya Kiangazi na masika .Aidha pia amewashauri waanze kulima kwa kitaalamu zaidi ili wapate mazao ya kutosha.pamoja na kuwaeleza yote hayo lakini pia akawasisitizia umuhimu wa kujiunga kujiunga kwenye vyama vya ushirika na kuacha tabia ya kuuza mazao yote kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu inayoweza kupelekea maeneo mengi kukosa chakula.

Akizungumza na wakulima wa Bonde la Mto katengera jana wakati wa ziara yake , vijiji vya Kinonko,Nyamibuye na Rumashi Ndagala alisema wakulima wengi wamekuwa na tabia ya kuuza mazao yote na kupelekea kubaki wakilia njaa baada ya mazao yao waliyo lima kuisha ,pia wakulima wanatakiwa kuunda vikundi vya ushirika vitakavyo wasaidia kupata mikopo,pembejeo na masoko yatakayo wasaidia kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu.

Alisema Wakulima wakiweza kulima misimu yote miwili ya Kiangazi na masika,bonde hilo lina uwezo wa kuhudumia wananchi wote wa Kakonko kutokana na mkulima mmoja kuwa na uhakika wa kulima hekali moja na kuzalisha gunia nane  za mpunga kwa msimu mmoja wa mavuno na hali inayo weza kuikomboa wilaya hiyo isikumbwe na janga la njaa.

Aidha Ndagala amewaomba maafisa kilimo wa Wilaya hiyo kuwawezesha wakulima kulima kwa misimu miwili na kuwapa mbinu za kulima kitaalamu kwa kutumia pembejeo zinazotolewa na Serikali, ili kuweza kupata Mazao mengi na kuweka tahadhali kutokana na hali ya hewa inayo weza kupelekea ukosefu wa mvua.

"Nniwaombe wananchi kwa mwaka huu mlime mazao yanayo weza kustahimili ukame kama Vile mihogo, mtama na viazi na yale yanayo stawi haraka kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi iliyojitokeza, hali inaweza kusababisha mwaka huu chakula kika kosekana kabisa, pia mjenge tabia ya kuhifadhi chakula msikiuze chote tusije tukaanza kuomba misaada wakati uwezo wa kuhifadhi chakula tunao",alisema Ndagala.

Kwa upande wake Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,Muhdin Alfani alisema bonde hilo lina zaidi ya kilomita 29 na linawakulima 310 na mradi wa kukamilisha ujenzi wa bonde hilo la umwagiliaji ni shilingi milioni 312 na kila hekali moja linaweza kuzalisha gunia 18 kwa msimu mmoja wa kilimo.

Alisema lengo la Halmashauri  kuanzisha mradi huo ni kuwasaidia wananchi wa Wilaya hiyo kulima na kupata mazao ya kutosha yatakayo wasaidia kuilisha wilaya na Nchi jirani ya Burundi ambayo inategemea chakula kingi kutoka kwa Watanzania katika masoko ya ujirani mwema na kuweza kuiongezea serikali pato la taifa.

Nao baadhi ya wakulima wa bonde hilo,Issa Masumo na Shedrack Milembe wameiomba Halmashauri hiyo kuwawezesha kupata masoko na kupangiwa bei maalumu itakayo wasaidia kuepukana na unyanyasaji wa Wafanya biashara wanaokuja kununua mpunga na kuwapunja wakulima na kukosa haki yao ya msingi wao kama wakulima. 

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ,akizungumza jambo na baadhi ya wakulima walioko katika bonde la Katengele,wakati alipokuwa akikagua kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Katengela kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.Dc Ndagara aliwaeleza wakulima hao kuwa kuanza kulima mazao yao kwa misimu miwili ya Kiangazi na masika kitaalamu zaidi na kujiunga kwenye vyama vya ushirika na kuacha tabia ya kuuza mazao yote kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu inayoweza kupelekea maeneo mengi kukosa chakula. 
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ,akiwasikiliza baadhi ya  wakulima walioko katika bonde la Katengele,wakati alipokwenda kukagua kilimo cha umwagiliaji katika Bonde la Katengela kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.
DC Ndagala akishiriki kulima kwenye moja ya shamba linaloandaliwa kwa ajili ya kilimo cha Mpunga,katika Bonde la Katengela kijiji cha Kinonko Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.


Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagaa ,akipima kina cha maji yanayotumika katika kilimo cha umwagiliaji kwenye bonde la Katengele,wakati alipokuwa akikagua kilimo cha umwagiliaji katika Bonde hilo kijiji cha Kinonko, Wilayani Kakonko katika mashamba ya Mpunga,mkoani Kigoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...