Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akizungumza na wakazi wa kata ya
Msongola katika ziara za kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika
wilaya hiyo.
Mtendaji
mkuu wa Kampunia ya upimaji na uuzaji Viwanja ya Tanzania Remex, Ali
Hamadi, akiwaonyesha baadhi ya wakazi wa kata ya Msongola ramaninya
mipango miji katika eneo hilo .
Katibu
tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogoro, akizungumza na wananchi wa
Kata ya Msongola wakati wa ziara ya kutatua kero za wananchi katika
maeneo yao .
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
MKUU
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesikiliza kero 126 za wananchi
wakati wa ziara yake katika kata tatu za Vingunguti, Pugu, Gongolamboto
na Msongola na kuipa wiki tatu kampuni ya Tanzania Remix kuwapatia
wananchi hati zao za viwanja.
Mjema
amesema kuwa wananchi hao wamesubiri kwa miaka mitatu sasa juu ya
mpango huo bila kuona matumaini, hivyo hakuna haja ya kuendelea
kusubiri.
"Sasa
natoa wiki tatu kuhakikisha fidia za wenye viwanja zinapatikana na
baada ya wiki mbili kila mmoja awe amepatiwa hati yake ambayo
itamuwezesha kuuza au kukopa katika mabenki mbalimbali"amesema Dc Mjema.
Dc
Mjema pia alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha
wanasimamia ulinzi katika kata ya Msongola kutokana na kukithiri kwa
vitendo vya uporaji na mauaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...