Na Mathias Canal, Singida

Wananchi wametakiwa kuachana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wanasiasa kwa kuwataka kutochangia shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia ujenzi wa maabara kwani kufanya hivyo ni kuwapumbaza wananchi ilihali wanasiasa hao wanaofanya hivyo wamesoma na kufikia kuwa na nafasi nzuri kwenye serikali ambapo pia watoto wao wana elimu nzuri na wengine wanasoma nje ya nchi.

Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu katika ziara yake ya kikazi iliyoanza leo katika Kata mbili za Kikio na Kata ya Misughaa.

Dc Mtaturu amewataka viongozi hao kutoyakimbia maeneo yao ya kazi ikiwemo majimbo na kuachana na uongozi wa sifa zisizokuwa na tija badala yake wanapaswa kurejea Katika maeneo yao ya utendaji ili kushiriki kwa pamoja na wananchi katika shughuli za Maendeleo.

Mraturu ambaye ameanza ziara hiyo ikiwa na engo la kutembelea miradi ya maendeleo na kujua maeneo yote anayofanyia kazi, Kuhimiza shughuli za Maendeleo na kuwakumbusha wanasiasa kuwa uchaguzi mkuu ulifanyika Octoba 25 Mwaka jana na kumalizika hivyo wakati huu ni wa kufanya kazi na kuzikabili changamoto zinazowatatiza watanzania kwa miaka mingi.

Amesema kuwa serikali inaposema wananchi wachangie shughuli za maendeleo haina maana kwamba wananchi wachangie pesa pekee bali wanaweza kuchangia mchanga, Tofali na nguvu zao katika kuhakikisha Vitongoji na Vijiji vyao vina imarika katika miradi mbalimbali yenye tija katika jamii.

Dc Mtaturu amewataka wanasiasa kutojificha kwenye kichaka cha Demokrasia huku hawana nidhamu badala yake kuihubiri demokrasia kwa kufanya shughuli za kuwawezesha wananchi kuimarika katika shughuli mbalimbali zitakazo wawezesha kuondokana na umasikini uliokithiri nchini Tanzania.

Ameahidi kuwavalia njuga baadhi ya wataalamu wote walioajiriwa na serikali kwa ajili ya kuwatumikia wananchi lakini wamebadili muelekeo na kuanza kufanya shughuli za siasa badala ya kuzitendea haki taaluma zao katika kuyafikia matokeo makubwa ya kipato cha wananchi.

"Watumishi wote wa serikali, Wakuu wa idara na vitengo pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wanapaswa kufanya kazi moja tu ya kutafsiri kwa vitendo ilani iliyoshika hatamu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)" Alisema Mtaturu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua jinsi ujenzi wa maabara unavyosuasua katika shule ya sekondari Mkunguakihendo ambapo amemuagiza Diwani kusimamia ujenzi huo uli kufikia mwakani maabara ianze kutumika
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua utengenezaji wa Chumvi katika Mbuga ya Mwakilongo iliyopo Kijiji cha Itagata, Kata ya Kikio
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua ujenzi wa shule ya Awali na Msingi Simbikwa.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu, akiwakwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Wakuu wa Idara na Vitengo, Diwani wa kata ya Kikio Steven Sinda, Walimu na Viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata ya Mkunguakihendo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...