Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Chistopher Ngubiagai, ametoa siku 14 kwa wavuvi haramu katika wilaya hiyo wajisalimishe na kukabidhi dhana wanazotumia.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la uchomaji wa zana za uvuvi haramu lililofanyika mjini Kilwa Masoko.

Ngubiagai alisema uvuvi haramu nitatizo linalohitaji nguvu na jitihada zinazotokana na uzalendo ili kulikabili. Kwasababu ya mbinu zinazotumiwa na wahalifu katika kuhakikisha hawakamatwi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema mapambano hayo ni makali na magumu, kwa sababu baadhi ya wahalifu hao kuwa na mtandao mkubwa unaowahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa umma wasiowaadilifu. Hivyo wilaya hiyo imetengeneza mikakati madhubuti itakayotokomeza tatizo hilo linalotishia uwepo wa viumbe hai wa baharini. 

Ngubiagai aliitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kuhakiki wavuvi wote waliopo katika wilaya hiyo na maeneo wanayofanyia shugulizao, kusajili vyombo vyote vya uvuvi na kuvipa namba za utambuzi na kujua kila chombo mahali kilipo, kuwasajili wavuvi wote walio kwenye kambi za uvuvi na kuainisha bandari maalumu zinazoshushia mazao ya uvuvi ya maeneo mbalimbali.

"Napenda kuwatahadharisha wasalimishe zana zao za uvuvi haramu haraka iwezekanavyo ndani ya wiki mbili kwani zama zao zimekwisha. Vita hii niliyoianza haitasimama nitahakikisha uvuvi haramu unatokomea kabisa katika wilaya hii,lengo ni kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinavinufaisha hata vizazi vijavyo," alisisitiza Ngubiagai.

Alibainisha kuwa kupitia hatua za awali za mapambano hayo ambayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli aliyotoa hivi karibuni jijini Mwanza, naya waziri mkuu, Kassim Majaliwa aliyotoa wilayani Mafia mkoa wa Pwani.

Wamefanikiwa kukamata kilo 281 za unga wa kutengenezea mabomu tambi 7, vibati 7 na chupa za mabomu ambazo zilikamatwa kutokana na ushiriano mkubwa wa raia wema kwenye kambi za uvuvi za Nyuni, Ukuza na Simaya.
"Unga uliokamatwa ulikuwa na uwezo wa kutengeneza chupa za mabomu 188,kila chupa ingeweza kuharibu eneo lenye ukubwa wa zaidi ya mita hamsini,maana yake nikwamba zisingekamatwa basi eneo la bahari lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 9400 zingeharibiwa kabisa," alisema.

Mkuu huyo wawilaya alitoa wito kwa serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kwa kusema "Kuna umuhimu wakuangalia na kutafuta uwezekano wa kuunda kikosi maalum cha kwa ajili ya kupambana na wavuvi haramu katika bahari na maziwa,kwa sababu hawa askari ingawa wanajitihidi sana na juhudi zao zinazaa matunda,lakini hawana uelewa mkubwa wa mambo ya bahari na sheria zake," alisema.

Kwa upande wake ofisa uvuvi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Ahmad Mkali. Alisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazosababisha kupunguza kasi ya kupambana na uvuvi huo ni uchache wa boti za kufanyia  doria.Akibainisha kuwa halmashauri hiyo inaboti moja tu. Wakati mahitaji halisi ni angalau boti nne."Wavuvi haramu wanavua bahari kuu ni mbali,na eneo la bahari nikubwa sana kwa boti moja inakuwa vigumu kuyafikia maeneo yote kwa wakati mmoja," alisema Mkali.
Baadhi ya zana haramu za uvuvi zilizokamatwa, Pichani ni Mabomu yanayotumika kulipulia Samakina viumbe vingine Baharini.

Zana Haramu za vuvi zikiteketea kwa moto. (Picha na :Bernad Mpangala Mchambuzi wa Mifumo Kilwa.)
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndg; Christopher Ngubiagai akizungumza na wavuvi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...