Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji katika mahafali ya saba yaliofanyika Oktoba Mosi katika viwanja vya Bodi jijini Dar es Salaam. 
Na Ismail Mohamed.
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amewataka Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wasiingiliwe katika taaluma zao na kwamba wanapaswa kuheshimiwa ili waweze kutoa huduma bora.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri huyo kwenye mahafali ya saba yaliofanyika Oktoba Mosi katika viwanja vya Bodi jijini Dar es Salaam.

Dk Kijaji amesema Serikali ya Awamu ya Tano, haitamvumilia mtu yeyote atakayetumia elimu aliyoipata kwa gharama za walipa kodi kwa kufanya kazi kwa manufaa binafsi  na kufuja mali za umma.

“Fani hii ina tija na ina mchango mkubwa katika taasisi husika na taifa kwa ujumla, Fani hii inapaswa kupewa heshima yake Kama vile wataalamu wa fani zingine wasivyoingiliwa katika utendaji wao, hivyo basi naagiza kuwa wataalamu hawa nao wasiingiliwe kwenye utendaji wao wa kitaaluma. Kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na ukiukaji wa sheria namba 23 ya mwaka 2007 na pia inawanyima wasifanye kazi zao kwa uhuru na kufuata misingi ya sheria na taaluma.

“Yeyote atakayepatikana akikiuka maadili ya kazi atachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweka fundisho kwa wengine na kuimarisha nidhamu katika utumishi wa umma. Mnapaswa kusoma kwa makini, Sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na kanuni zake iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016 ili kujua madhara ya kukiuka taratibu za ununuzi,” amesema Dk Kijaji.

Naibu waziri huyo amewataka wahitimu hao kutatua matatizo ya manunuzi holela na kuepuka kuingia kwenye mikataba mibovu ya ununuzi. 

Pia, amewataka wahitimu hao kuepuka vitendo vya rushwa katika ununuzi na ugavi kwani sheria zipo na kwamba zitatumia kuwabana endapo hawatazingatia sheria za ununuzi na ugavi. 
“Itakuwa ni aibu kwa fani hii ikiwa mtaalamu mmoja atabainika kuhusika na vitendo vya rushwa . Nawasihii sana, zingatieni kanuni za maadili mlizopewa  leo,”amesema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi, Dk Hellen Bandiho amesema mahafali hayo ni ya saba tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo na kwamba bodi hiyo inaendelea kusimamia na kukuza fani ya ununuzi na ugavi nchini.

Dk Bandiho amesema kuwa kati ya watahiniwa 81,771 waliofanya mitihani, 27,814 wamefaulu. Pia, amesema kwamba mafunzo yanayotolewa na bodi hiyo yamekuwa yamekuwa yakifanyiwa mapitio mara kwa mara na kurekebishwa ili kuhakikisha kwamba mafunzo yanayotolewa yanakidhi mahitaji ya sasa.

“Bodi kwa kushirikiana na vyuo vya mafunzo ya elimu ya juu imehimiza kuanzisha mafunzo mathubuti yanayohusu fani ya ununuzi na ugavi vyuoni ambapo zaidi ya vyuo 20 hapa nchini hivi sasa vinatoa shahada ya kwanza ya taaluma ya ugavi na baadhi shahada ya pili nay a tatu. Hatua hii inawezesha fani yetu kupata wataalamu wenye ubora wa juu kielimu,” amesema Dk Hellen Bandiho.

Katika mahafani hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred Mbanyi amesema kuwa bodi hiyo ina jukumu la kuwasajili wataaluma na kuratibu mienendo ya wanataaluma kupitia miongozo ya maadili, mafunzo endelevu , kuwapa leseni wanataaluma wanaokidhi matakwa na kaguzi za kitaaluma.

“Katika kipindi cha kuanzia Julai 2015 hadi Juni 2016, Bodi imedahili na kuendesha mitihani ikiwa ni moja ya jukumu lake kisheria kwa wanafunzi3,327 katika ngazi za cheti cha awali, Cheti Msingi na Shahada ya ununuzi na ugavi ambapo kati yao 1,754 wamefaulu katika ngazi mbalimbali,” amesema Mbanyi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...