THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DKT. CHARLES MWIJAGE AITAKA NBS KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO KUFANYA TAFITI YA VIWANDA VIDOGO NCHINI

Na Beatrice Lyimo -MAELEZO-Dar es Salaam 

SERIKALI imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini NA Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.

Dkt Mwijage alisema kuwa katika mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.

Alisema katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia kuinua uchumi wan chi.

“Asilimia 25- 40 ya mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao yao” alisema Mwijage.
Wazi wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu mbalimnbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto) akimkabidhi taarifa ya kitabu cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. 
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
 (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)