THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

DKT MGWATU AWATAKA WATENDAJI KUZIBA MIANYA YA UPOTEVU WA MAPATO TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) akizungumza na watumishi wa TEMESA Kilimanjaro alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) akiangalia “honing machine” inayotumika kwa ajili ya matengenezo ya vipuli vya magari kituoni hapo, katikati ni Bw Firmin Lyaruu na Meneja Mhandisi wa TEMESA Kilimanjaro Bw. Alfred Ngw’ani.

Na Theresia Mwami- TEMESA Kilimanjaro.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watendaji kuziba mianya ya uvujaji wa mapato, ili kuhakikisha Wakala unakusanya mapato iliyokusudia na kufanya matumizi stahiki kwa maendeleo ya Wakala.

Amesema hayo wakati akizungumza na  na watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanajaro alipotembelea na kujionea hali ilivyo katika kituo hicho na kuwahimiza watumishi wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja na kutoa huduma zenye ubora.

“Nawaomba muwe na  mbinu mbadala yakuzuia mianya ya uputevu wa mapato na  mzibane Taasisi mnazozidai  walipe madeni ili mapato yatakayokusanywa yasaidie kuboresha zaidi karakana zetu.” Alisisitiza Dkt. Mgwatu.

Nao watumishi wa kituo cha TEMESA Kilimanjaro kwa nyakati tofauti, wamemuahakikishia mtendaji huyo kufanya kazi kwa kujituma na kuzidi kupambana kuipeleka mbele TEMESA ingawa kumekuwapo na  ukosefu wa vitendea kazi  kulingana na taaluma mbali mbali zilizopo kwenye kituo hicho.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vilivyopo kanda ya Kaskazini kuangalia utendaji kazi wake na kuona changamoto zilizopo ili ziweze kupatiwa ufumbuzi kwa maendeleo ya Wakala huo.