Na Theresia Mwami TEMESA Arusha.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt Mussa Mgwatu ameahidi kuziimarisha karakana zilizopo chini ya TEMESA ili kuimarisha utendaji kazi.

Mikakati hiyo imetolewa leo na Mtendaji huyo alipokutana na watumishi TEMESA wa mkoani Arusha alipotembela kituo hicho kuangalia utendaji kazi wa kituo hicho.“Naahidi kushirikiana nanyi katika kuijenga TEMESA Mpya na naomba ushirikiano wenu na muwe wafuatiliaji wa mambo kwani kazi zetu zinahitaji sana ufuatiliaji wa kina” Alisema Dkt Mgwatu.

Ameongeza kuwa amepanga mikakati namna ya kuyatambua madeni ya TEMESA pamoja na utunzaji wa taarifa zake, kufanikisha utendaji kazi wa baadhi ya karakana,kuwezesha urahisi wa mawasiliano kati ya TEMESA makao makuu na vituo mikoani.Amesisitiza kuwa watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa dhana potofu iliyojengwa juu ya TEMESA kwa wateja wake kuwa wanafanya kazi kwa mazoea, wajiimarishe katika utendaji kazi kwa kasi, ubora, weledi uadilifu, ufuatiliaji, na uwajibikaji.

Katika hatua nyingine Dkt. Mgwatu ametembelea Chuo cha Ufundi Arusha ili kujionea shughuli mbalimbali za mafunzo yanayotolewa chuoni hapo na amefurahishwa na vifaa vya kisasa vya kutengenezea magari vinavyotumika katika karakana ya chuo hicho kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wake.Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Richard Masika alionesha nia ya kushirikiana kwa ukaribu na TEMESA ili kuweza kuboresha mafunzo ili kupata huduma zinazotolewa katika karakana za TEMESA.

Dkt. Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi kutembelea vituo vya TEMESA Kanda ya Kaskazini ili kujionea changamoto na hali halisi ya utendaji kazi wa vituo hivyo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme- TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) akiwaelekeza jambo watumishi wa TEMESA Arusha alipotembelea kituoni hapo kutoka kushoto waliosimama ni Meneja wa TEMESA Arusha Mhandisi Heriel Mteri, katikati ni Mhasibu wa TEMESA Arusha ndugu Simon Ringia na kulia ni Mhasibu Msaidizi wa TEMESA Arusha Bi. Rebecca Temba.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Karakana ya Magari chuo cha Ufundi Arusha, Bw. Joseph Kotini wakati alipotembelea chuo hapo.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(kulia) pamoja na Mkuu wa Karakana ya Magari chuo cha Ufundi Arusha Bw. Joseph Kotini wakiangalia shimo linatumika kukagua na kufanya matengenezo madogo ya magari chuoni hapo.
Mkuu wa Karakana ya Magari Chuo cha Ufundi Arusha Bw. Joseph Kotini (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu juu ya mtambo unaotumika kufanya ukaguzi na matengenezo makubwa ya magari chuoni hapo.Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...