Na mdau. Sweden
FC Kilimanjaro ni timu ya soka inayoundwa na Watanzania waishio  Sweden. Kama sikosei, hii ni timu ya kwanza kabisa inayomilikiwa na Watanzania  popote ughaibuni kushiriki kwenye mfumo rasmi wa ligi ya soka kwenye nchi za ughaibuni. Timu hiyo juzi imeandika historia nyingine kwa kuchukua ubingwa wa daraja la saba la ligi ya Sweden na kupanda hadi daraja la sita.
Safari bado ndefu lakini haya tayari ni mafanikio makubwa yanayotokana na juhudi za pamoja na  wana-Diaspora wa Sweden za kudumisha mshikamano, kuitangaza nchi yetu kupitia sports na kutengeneza fursa za baadaye za vijana wa Kitanzania kuja kukuza vipaji na kucheza soka Ulaya.Kwa kweli vijana hawa wanastahili support na pongezi zenu za dhati...
 FC Kilimanjaro
 FC Kilimanjaro wakishangilia kupanda daraja
 Mashabiki wa FC Kilimanjaro
 Furaha ya kupanda daraja
habari ndiyo hiyo, wanasema wadau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...