THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

GLOBAL ILIPOWATEMBELEA WAFUNGWA GEREZA LA UKONGA DAR ES SALAAM


Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya tamasha la michezo mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.

Akiongea katika tamasha hilo, Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi, Eric Shigongo, amewaambia wafungwa kuwa dhamra ya ujio wao gerezani hapo ni katika kuonyesha kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao gerezani siyo kwamba wametengwa na dunia.

Shigongo aliwatia moyo wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya kubadilika na kuwa raia wema.“Kila mwanadamu anao wajibu wa kubadili maisha yake, Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi na wewe na kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka, kwa nini wewe ushindwe?” aliuliza Shigongo.

Aliongeza: “Najua wengi wenu mko hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwa kuwa mmehukumiwa, hizi ni hukumu za wanadamu, mnao uwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku mkitoka duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili maisha yako, kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu atakuongoza."

Wadau wengine walioungana na Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na Rajab Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza hilo la Ukonga) ambao kwa pamoja walileta zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao vikiwemo vifaa kama sabuni, soda na kikombe ambacho kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika mpira wa miguu.

Katika tamasha hilo wafungwa walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika kijiko, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti, kuvuta kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya uchekeshaji, kuimba kwa mtindo wa kufokafoka, ngoma za jadi na burudani kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta.

Picha zote na ASP Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza.

Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (aliyesimama), akiwasalimia wafungwa (hawapo pichani) wa gereza la Ukonga katika Tamasha la Kuadhimisha Siku ya Nyerere (Nyerere Day) Oktoba 14, Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitia saini kitabu kitabu cha wageni gerezani Ukonga katika Tamasha la Michezo wakati wa kuadhimisha Nyerere Day. Kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Stephen Mwaisabila, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Thom Nyanduga, Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo na Abdalah Mrisho ambay ni Meneja wa Global Publishers.

Johnson Nguza aka Papii Kocha (wa pili kushoto) akitumbuiza na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa tamasha hilo.
Baadhi ya wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia kwa magunia katika tamasha hilo.