Ziafuatazo
ni picha za hafla mchapalo (Cocktail Party) ya kukata na shoka ya
kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa Mataifa tangu ulipoanzishwa
iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez jijini
Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kuhudhuriwa na wageni
mbalimbali mashuhuri kutoka taasisi mbalimbali za serikali, binafsi
pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa
katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya umoja huo tangu
kuanzishwa kwake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo
pichani) kuzungumza na wageni waalikwa.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika hafla mchapalo ya kusheherekea miaka 71 ya Umoja wa
Mataifa iliyofanyika nyumbani kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez
(kulia) jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia)
akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake na wageni waalikwa kwenye hafla
hiyo.
Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...