Mkurugenzi Mtendaji  wa Hakielimu, John Kalage, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya hatua zilizo chukuliwa na Serikali kwa Walimu wa Mbeya Day.

Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii.
TAASISI isiyo ya kiserikali inayosimamia mwenendo wa Elimu hapa nchini ya Hakielimu imeipongeza Serikali kwa hatua za kinidhamu zilichokuliwa kwa wale wote waliohusika kutoa adhabu ya kikatili kwa mwanafunzi wa kidato cha 3 ,Sebastian Chinguku wa shule ya sekondari ya Mbeya day.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dare s Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa wa tasisi hiyo, John Kalage amesema kuwa  wamepokea tarifa hiyo kwa masikitiko makubwa sana mara baada ya kuona ukatili uliopotiliza.

“tunaipongeza Serikali kwa kuchukua hatua za awali zikiwemo kuliagiza Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua za haraka dhidi ya wanafunzi waliokuwa wanafanya mazoezi ya kufundisha waliohusika katika tukio lile. Aidha tunampongeza Mwalimu aliyethubutu kukemea na kufichua ukatili huu uliopotiliza hivyo tunaomba mamlaka husika zichukue hatua madhubuti za kulinda uhai hata ajira ya mwalimu huyu jasiri” amesema Kalage.

Ameongeza kuwa Hakielimu inaitaka Serikali kuhakikisha suala hili linashughulikiwa kwa upana wake na kuendelea kuitaharifu jamii juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya waliohusika na ukatili huu.

Alimaliza kwa kusema kuwa licha ya tukio la Mbeya linaonekana kuchukua mjadala mpana hapa nchini kwa sasa, tunapenda kuitaharifu serikali kuwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto wa mwaka 2011 imeonesha kuwa kuna ukatili wa kutisha sana kwa watoto katika shule nyingi hapa nchini vikiwemo vya kimwili na kingono.

Aliweka wazi kuwa adhabu kama hizi zinapotolewa kwa watoto, husababisha wato kutafuta namna ya kukwepa adhabu hiyoo na kupelekea kukimbia masomo yao na hatimaye kuacha shule kabisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni kweli kuna shule nyingi hapa nchini ambazo zimekuwa zikitoa na zinaendelea kutoa adhabu za namna hii kwa wanafunzi. Uchunguzi zaidi unatakiwa kufanywa ili kuwafichua siyo tu wale waliotoa adhabu hizo bali hata wanafunzi ambao waliathirika kiafya na kisaikolojia. Hao waalimu waliohusika kumpiga mwanafunzi inabidi wafutiwe kabisa vyeti vya ualimu na watumikie kifungo cha muda mrefu ili uwe mfano kwa wengine wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...