Na Alda Sadango, Afisa habari Wilaya ya Handeni.
Viongozi  wa halamshauri ya wilaya ya Handeni na Kilindi wamefanya ziara ya kwenda kutatua mgogoro wa mpaka wa kijiji cha Gole kilichopo wilayani Handeni na Negelo kilichopo wilayani kilindi.

Ziara hiyo iliofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba
8,2016,imefamyika kufuatia kijiji cha Gole kulalamika kuwa kuna muwekezaji anafanya shughuli za kilimo na ufugaji katika eneo la hifadhi ya msitu wa kijiji uliotengwa tangu 2011.

Wakuu wa wilaya ya Handeni na Kilindi sambamba na Wakurugenzi wa wilaya hizo walifika eneo la mgogoro huo wakishirikiana na wataalamu kutoka pande zote mbili,na kusoma ramani iliyotumika kutenganisha mipaka ya wilaya na vijiji.

Mgogoro ulimalizika baada ya wataalamu hao wa mambo ya ramani, kutoa umiliki halali wa eneo aliyopo muwekezaji kuwa ni ndani ya Kijiji cha Gole.Wataalamu hao walieleza kuwa  Sheria,taratibu na kanuni zitafuatwa katika kumuondoa muwekezaji huyo katika eneo hilo la hifadhi ili aweze kufanya shughuli zake za kiuchumi katika eneo husika kulingana na mpango bora wa ardhi.

Aidha uongozi uliwataka wataalamu wa pande zote mbili kukaa ndani ya siku kumi kuanisha mipaka inayotenganisha vijiji vya wilaya ya Kilindi na Handeni ili kuondoa utata kwenye vijiji vingine vilivyo na utata.
Mkuu wa wilaya ya Handeni,Mh. Godwin Gondwe akifafanua jambo kwa wananchi, Mh Gondwe aliwaeleza Wananchi hao kuwa dhamira kuu ni kuhakikisha kwamba amani inatawala pande zote mbili na kuhakikisha shughuli za kimaendeleo zinasonga mbele na kwamba hakuna mwanachi yeyote anayekatazwa kwenda kijiji kingine kufanya shughuli za kiuchumi,kikubwa ni kufuata sheria, taratibu na kanuni za mahali husika.
Wakuu wa wilaya Mh. Godwin Gondwe na Mh. Sauda Mtondoo pamoja na wananchi wakikagua na kujionea hali halisi ya eneo ambalo mpaka unapita, na eneo ambalo mwekezaji amechimba bwawa la maji kwa ajili ya mifugo yake.
Wataalamu wa ardhi kutoka halmashauri zote mbili Handeni na Kilindi wakitoa ufafanuzi wa mgogoro huo wa mpaka,kwa wananchi .
Mkuu wa Wilaya ya Handeni ,Mh. Godwin Gondwe akipeana mkono na Mkuu wa Wilaya ya Kilindi,Mh. Sauda Mtondoo kuonesha ishara ya kupongezana kwa kuelewa alama za mipaka ya maeneo yao ya kiutawala.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...