THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

HUZUNI: KIJANA SAID ALLY ALIYETOBOLEWA MACHO NA SCORPION HAWEZI KUONA TENA...

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  leo ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana Said Ally (anayemfariji juu pichani) aliyetobolewa macho na mtuhumiwa aitwaye Scorpion maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena. Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema:

"Nianze kuwashukuru ndugu zangu wa Clouds hasa kipindi cha #LeoTena kwa sauti zao mpaka kumfikia ndugu yetu Said ambaye alitobolewa macho kinyama na  kwa sasa haoni tena.... 
"Majibu ya daktari yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi.  Majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote.

"Serikali ya Mkoa wa Dar es salaam imejitolea k
umpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena.

"-•Kumpatia Elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira.
"-•Serikali ya Mkoa imetoa Gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake.
"-•Vilevile Serikali yetu itatoa kiasi cha Shilingi milioni 10 kama sehemu ya Mtaji. Kabla ya kupatwa na ulemavu Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwa kuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja".

#KutokaOfisiYaMkuuWaMkoa
Said Ally akifarijiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Mhe. Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam Mhe. Paul Makonda katika majonzi.
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


Kuna Maoni 4 mpaka sasa.

 1. HK Anasema:

  Pole sana ndugu yetu Bw. Said Ally kwa mithihani yote iliyokukuta pasina kutarajia, hujafa kweli hujaumbika. Pole sana sana na khasa kwa khabari ambazo naamini wengi wetu siyo wewe pekee tu, zimetuhuzunisha sana na kutusikitisha, ambapo pamoja na jitihada zote zilizofanywa na wataalam husika, ili kuhakikisha kuna uwezekano wa kuweza kuona tena, lakini siyo rizki, zimethibitisha uwezekano huo wa kuweza kuona tena haupo, pole sana sana ndugu yangu, yote ni mithihani yake Mwenyeez Mungu na juu ya kila jambo ana makusudio yake. Lakini isingekuwa kwa kitendo kama hicho ulichotendewa cha kinyama kabisa kilichotendwa na huyo katili Scorpion. In Sha Allah Mwenyeez Mungu atakuhifadhi,kukulinda, kukuongoza na kukusaidia kwa kila hali. Nyamaza kulia na In Sha Allah MOLA atakupa faraja, nguvu, stahmala na uvumilivu, Mwenyeez Mungu ni mwingi wa rehma na ana kudura zake kwa kila liwafikalo waja wake, hakupi kilema akakunyima mwendo. Madhali pumzi bado unayo, basi usikate tamaa na kuvunjika moyo, kwa Muumba hakuna lishindikanalo, japo hutoweza kuona tena, basi In Sha Allah atakuongoza mithli ya anavyowaongoza waja wake wote wenye upungufu huo wa kuona. Pole sana na tunakuombea uwe ni mwenye siha njema na maisha mema, mazuri ya furaha na amani kabisa, In Sha Allah.

  Pia shukran za dhati na za peke kwa Mh. Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam. Bw. Paul Makonda. Kwa kweli amekuwa ni faraja kubwa na mfatiliaji wa karibu sana na namekuwa ni mchango mkubwa kwa yote yaliyompata ndugu yetu Bw. Said Ally. Amejitahid kwa hali na mali kufuatilia kwa wataalamu husika kwa kadri awezavyo, ili kutaka kufaham na kuhaakikisha ni ipi khatam ya uwezekano wa Macho ya Bw. Said Ally kuweza kuona. Lakini kwa bahati mbaya imethibitika kutowezekana kwa macho ya Bw. Said Ally kuweza kuona tena. Mwenyeez Mungu akupe moyo huo huo wa imani, upendo na huruma kwa wananchi wa Mkoa wako na Taifa zima kwa jumla. Ni kiongozi unaejali utu na pia unaetenda kwa vitendo na uliyemfano bora wa kuigwa. MOLA akuongoze katika majukumu yako na maisha yako ya kila siku kwa jumla, kwenye mema akukurubishe nako na penye shari zote akunusuru na kukuepushia. In Sha Allah-Ameen.

 2. Anonymous Anasema:

  Jamani kweli kabla hujafa hujaumbika... Poleni mno wanafamilia na mungu awazidishie nguvu katika kipindi hiki kigumu .. Said pole baba mtihani wako ni mgumu sasa uanze kujifunza kuishi bila kuona jamani.

  SASA HUYO SCORPION MBONA ANAKUWA KAMA HERO IN THIS JE AMESHAKAMATWA MAANA ANAJULIKANA ANAPASWA KUNYONGWA HAFAI KATIKA JAMII ATAENDELEA KUUMIZA WENGI

 3. Anonymous Anasema:

  Huyo scorpion hakai porini lazma anakaa mtaani...hapo mtaani Kuna mwenyekiti wa mtaa hilo eneo Lina diwani na viongozi wa serkali za mitaa. Nasikia huyo mbwa anajulikana kwa ikatili na amekuwa akiangaliwa tuu hai viongozi wawajibishwe na kufukuzwa kazi hats Kama wamechaguliwa...nadhani Kuna haha ya mwenyekiti wa mtaa awe wa kuteuliwa maana Ni kiungo muhimu Sana na serilali kuu. Vile vile polisi nao Ni wakulaumiwa maana mtu ukiwashitaki vijana wahuni wa mtaani wao wanaenda kuwakamata kuchikua pesa mbaya zaidi wanawaambia nani kawachoma...hii inapelekea mtu kuogopa kushitaki nadhani kiundwe kitengo maalum kwa mkuu Wa mkoa na wilaya ambacho kitakuwa kinapokea taarifa za watukutu wa mitaani badala ya hawa polisi

 4. Hope Anasema:

  Maoni yote mazuri na ninaungana nanyi wote kumpa pole nyingi muathirika. Pamoja na kuona masikitiko makubwa ya mkuu wa mkoa, Ningependa pia kusikia yeye anasemaje na ni kiasi gani ameyapokea haya kwani nafahamu kisaikolojia anateseka sana..