KAMPUNI ya IMPACTAFYA imezindua rasmi program ya Mazoezi Movement to Fitness kuhamasisha Watanzania kuwa na kaliba ya kufanya mazoezi kuepukana na matatizo yatokanayo na kutofanya mazoezi. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Idara ya  Habari MAELEZO, Mkurugenzi wa IMPACTAFYA, Bhakti Shah amewataka watanzania kuamka na kulichukulia suala la kufanya mazoezi kuwa jambo la kupewa kipaumbele. 

Alisema Tanzania iko hatarini kupoteza mamillioni ya watu ambao ni nguvu kazi ya jamii kwa kutofanya mazoezi, “Ugonjwa wa kisukari ambao kwa kawaida huwapata watu wazima unaongezeka kwa haraka ulimwenguni pote na sasa hata vijana wapo hatarini kwa sababu hawafanyi mazoezi, asilimia 20 hivi ya vifo vyote vilivyotokea miongoni mwa watu walio na umri wa miaka 21 hadi 45, vilisababishwa na kukosa kufanya mazoezi.” 

Alihoji kama Teknolojia Ni Baraka au Laana? Bhakti alisema “Leo watu wana afya bora na wanaishi muda mrefu zaidi kuliko wale walioishi karne nyingi zilizopita kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia ambayo imekuja na Vifaa vya kisasa vya matibabu, lakini ni teknolojia hiyo hiyo iliyoleta mashine ambazo zimesaidia kupunguza kazi nyingi ngumu na hivyo watu wengi waishi maisha ya kukaa tu bila kufanya mazoezi yakutosha.” alisema 

“Katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni yenye kichwa cha habari International Cardiovascular Disease Statistics, Shirika la Moyo la Marekani lilieleza kwamba “mabadiliko ya kiuchumi, watu kuhamia mijini, usitawi wa viwanda, na kuenea kwa biashara za kimataifa, na mitandao ya kijamii, imesababisha kuleta mabadiliko katika mitindo ya maisha ambayo huchangia ugonjwa wa moyo.” Ripoti hiyo inataja “kutofanya mazoezi na kula vyakula visivyofaa” kuwa mambo yanayochangia sana ugonjwa huo. 

Alisema Mtindo wa maisha wa leo wa mijini, mfanyakazi anaweza kuketi mbele ya kompyuta karibu siku nzima, aende mahali popote atakapo kwa gari lake, na atazame televisheni na kubrows kwenye mitandao ya kijamii jioni yote, na hivyo kujiingiza katika maradhi ambayo yamehatarisha maisha. 

“Watu wengi zaidi wanapendelea kutumia motokaa na pikipiki badala ya baiskeli, asilimia 25 ya safari zote hazizidi kilometa moja hivi, asilimia 75 ya safari nyingi fupi hufanywa kwa gari. Hii ni hatari” alisema. 
Mkurugenzi wa IMPACTAFYA, Bhakti Shah akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi rasmi wa program ya Mazoezi Movement to Fitness, kuhamasisha Watanzania kuwa na kaliba ya kufanya mazoezi kuepukana na matatizo yatokanayo na kutofanya mazoezi,Kulia ni mmiliki wa blog ya jamii 8020fashions,Shamim Mwasha ambaye ni  mmoja wa watakaokuwa wahamasishaji wakubwa kuhusiana na programu hiyo na shoto ni  mshauri wa masuala ya afya kwa Jamiii,Dkt Fred  Mashili. 
Mmiliki wa blog ya jamii 8020fashions,Shamim Mwasha ambaye ni  mmoja wa watakaokuwa wahamasishaji wakubwa kuhusiana na programu hiyo,akitoa ufafanuzi zaidi kwa Wanahabari namna ya uhamasishaji huo utakavyofanyika,shoto ni Mkurugenzi wa IMPACTAFYA, Bhakti Shah. 
Pichani kati Dkt Fred Mashili ambaye ni mshauri wa masuala ya afya kwa Jamiii na mmiliki wa Blog ya Jamii Health akielezea umuhimu wa kufanya mazoezi na namna ya kuijenga na kuilinda afya yako isikumbwe na magonjwa mbalimbali yatokanayo na kutokufanya mazoezi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...