NA VICTOR MASANGU, KISARAWE.

NAIBU waziri ofisi ya rais  Tamisemi Selaman Jafo amewaagiza maafisa elimu wa shule za sekondari na msingi hapa nchini  kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea ya kushinda wakiwa wamekaa ofisini tu bila ya kujishughulisha na badala yake wanapaswa kuhakikisha wanakwenda katika maeneo ya kazi hususan ya vijijini kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbali  zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa madawati, vyoo pamoja na madarasa.

Jafo ametoa agizo hilo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 150 kwa niaba ya serikali  katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani yaliyotolewa na umoja wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu (UWAMAMI) iliyofanyika wilayani humo.

Alisema kwamba kuna baadhi ya maafisa elimu hawatambua majukumu yao ipasavyo hivyo  kutokana na agizo lililotolewa na  Rais Dr. John Magufuli la wanafunzi wote kusoma wakiwa wamekaa chini ya madawati atahahakikisha anawavalia njunga watendaji wote  watakaobainika wanakwamisha kwa makusudi  juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

“Kwa kweli kuna baadhi ya maafisa elimu wengine wana tabia ya kukaa tu mezani hawaendi kujishughulisha na kuangalia changamoto za vijijini, ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya elimu hapa nchini kwa hiyo ninawaomba sana tucahpe kazi kwa bidii, ili tuweze kuleta maendeleo ya elimu,”alisema Jafo.
 Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi kushoto Seleman Jafo akipena mikono na Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wilaya ya Kisarawe,(UWAMAMI) baada ya hafla fupi ya kukabidhiana madawati 150 yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 15.
 Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi akizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 150 kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kuondokana na tatizo la kukaa chini (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...